1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyang'anyiro cha Madaraka baada ya Uchaguzi wa Ulaya

Oumilkheir Hamidou
27 Mei 2019

Vyama vikuu vya kisiasa vimepata pigo kubwa katika uchaguzi wa bunge la ulaya huku vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vikikosa wingi wa kura waliokuwa wakiutarajia. Walinzi wa mazingira na waliberali wanawika

https://p.dw.com/p/3JAt0
Symbolbild Europawahl
Picha: picture-alliance/AP Photo/F. Seco

Kwa mujibu wa matokeo  ya uchaguzi wa bunge la Ulaya yaliyochapishwa usiku wa  kuamkia jumatatu chama cha kihafidhina barani Ulaya EPP kinaendelea kudhibiti wingi wa viti, viti 179, ikilinganishwa na viti 216 katika bunge lililopita. Kutokana na hali hiyo wahafidhina hawajakawia kudai mgombea wao Manfred Werber wa kutoka Ujerumani akabidhiwe wadhifa wa mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya.

Wasoshial Democrat wanakamata nafasi ya pili katika bunge la ulaya kwa kujikingia viti 150 dhidi ya 185 ilivyopata mwaka 2014, wanapinga madai hayo wakiashiria uwezekano wa kuzuka majadiliano makali katika kinyang'anyiro cha kuanian nyadhifa muhimu katika taasisi za Umoja wa ulaya.

Ingawa vyama vya EPP na wasoshial Democrat wanasalia kuwa vyama vikuu katika bunge la Ulaya, hata hivyo wamepoteza uwezo wao wa kujikusanyia wingi mkubwa wa kura kuweza kuidhinisha miswaada yote inayopitishwa-hali inayoashiria mwisho wa enzi yao.

Walinzi wa mazingira washangiria matokeo yao ya uchaguzi wa bunge la Ulaya
Walinzi wa mazingira washangiria matokeo yao ya uchaguzi wa bunge la UlayaPicha: Getty Images/AFP/T. Schwarz

Walinzi wa Mazingira wana wika

Watabidi washirikiane na walinzi wa mazingira waliojizidishia idadi ya viti kutoka 52 na kufikia viti 70 na hasa kutokana na wingi wa kura walizojipatia nchini Ujerumani na Ufaransa. Waliberali pia kikiwemo chama cha rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamefanmya vyema na kujipatia viti 107 kutoka viti 69 katika bunge lililopita.

Rais huyo wa Ufaransa miongozi mwa viongozi wanaopigania ujenzi mpya wa umoja wa ulaya ameshindwa kwa ponti 0.9 ya kura  na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Marine Le Pen-Rassemblement National .

Marine Le Pen na chama cha La Ligue cha Matteo Salvini kilichoibuka na ushindi nchini Italia kwa kujikingia takriban thuluthi moja ya kura wanataka kuunda ushirika wa vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia, vyama vinavyouangalia kwa jicho la wasi wasi Umoja wa ulaya na vile vinavyopigania uzalendo ambao kwa pamoja wanashikilia viti 58 badala ya 37 katika bunge la mwaka 2014.

Marine Le Pen,mwenyekiti wa chama cha Ufaransa cha siasa kali za mrengo wa kulia
Marine Le Pen,mwenyekiti wa chama cha Ufaransa cha siasa kali za mrengo wa kuliaPicha: Reuters/H.-P. Bader

Licha ya kunyakua kura nyingi wafuasi wa siasa kali hawana nguvu

Hata hivyo itakuwa shida  kufikiria ushirikiano pamoja na chama cha Nyota tano cha Italia kinachotarajiwa kushirikiana na kile Brexit cha Nigel Farage wa Uingereza, aliyeibuka na ushindi wa asili mia 31.7, ikiwa ni sawa na viti 29 katika bunge la Ulaya.

Na hata wakichanganyika pamoja na makundi ya kihafidhina na yale ya siasa kali za kihafidhina, kutoka Uingereza na Poland, vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia vitakuwa na viti 172 tu dhidi ya viti 506 vya wahafidhina, wasocial Democrat, walinzi wa mazingira na waliberali. Bunge la Ulaya lina jumla ya viti 751.

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Reuters/SFP

Mhariri:Yusuf Saumu