1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Kim Jong Un aliamuru jeshi lake kukaa tayari kwa vita

28 Desemba 2023

Kim Jong Un leo ameamuru jeshi la nchi yake, kitengo cha zana za kivita na silaha za nyuklia kuharakisha maandalizi ya vita ili kukabiliana na kile alichokitaja kuwa makabiliano ambayo hajawahi kushuhudiwa na Marekani.

https://p.dw.com/p/4aec8
Korea Kaskazini | Gwaride la kijeshi mjini Pyongyang
Kombora la Korea Kaskazini aina ya Hwasong-17Picha: KCNA/KNS/AP/picture alliance

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un ameyasema hayo wakati akizungumzia mwelekeo wa kisera kwa mwaka mpya katika mkutano muhimu wa chama tawala jana Jumatano, na kuongeza kwamba Pyongyang itaongeza ushirikiano wa kimkakati na nchi zinazopinga ubeberu.

Korea Kaskazini imekuwa ikiimarisha mahusiano yake na Urusi miongoni mwa mataifa mengine huku Washington ikiishutumu Pyongyang kuiuzia Moscow zana za kijeshi kwa ajili ya oparesheni yake ya kijeshi nchini Ukraine, wakati Urusi ikitoa msaada wa kiufundi kwa Korea kaskazini kwaajili ya kuimarisha uwezo wake wa kijeshi.

Katika hatua nyingine Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol leo ametembelea jeshi katika upande wa mashariki mwa nchi kukagua maendeleo ya ulinzi na kuapa kutoa majibu ya haraka ikiwa kutotokea uchochezi wa aina yoyote kutoka kwa jirani yake Korea Kaskazini.