1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa LRA aahirisha kutia saini mkataba wa amani

Kalyango Siraj1 Aprili 2008

Kony asema atasaini wiki mbili zijazo

https://p.dw.com/p/DYnD

Serikali ya Uganda imepokea kwa shingo upande ombi la kiongozi wa kundi la uasi la Lord Resistance Army, LRA ,la kuahirishwa kwa tarehe ya kutia saini mkataba wa amani.

Sherehe hiyo ilikuwa ifanyike Ijumaa ya wiki hii mjini Juba,Kusini mwa Sudan lakini sasa imeahirishwa kwa wiki mbili zaidi.Duru za LRA zinasema hatua hii imechukuliwa kutokana na kuwa kiongozi huyo ni mgonjwa madai yaliyopingwa na serikali.

Serikali ya Uganda inasema imesikitishwa na hatua ya sasa ya kiongozi wa kundi la uasi la Lord resistance Army-LRA Joseph Kony ya kuahirisha kutia saini mkataba wa kuleta amani kaskazini mwa Uganda.

Mpango wa awali ulikuwa yeye angesaini saini kesho jumatano April 4 lakini anasema sasa hataweza kufanya hivyo hadi aidha tarehe 10 au 15 mwezi huu wa nne.Hatua yake hii inaonekana kama pigo katika juhudi za kumaliza mgogoro ambao umedumu miongo miwili ambapo watu maelfu kadhaa walipoteza maisha yao na wenghine takriban miliioni mbili kuachwa bila ya makao.

Henry Okello Oryem ni Waziri wa Uganda katika wizara ya mashauri ya kigeni anaehusika na ushirikiano wa kikanda na pia ni naibu mkuu wa ujumbe wa serikali ya Kampala katika mazunguzo na waasi hao mjini Juba.

Waziri asema wamesikitishwa na hatua hiyo kwani walikuwa wamejiandaa kutekeleza mambo mbalimbali walikuwa wamukubaliana hapo awali.

Ingawa wajumbe wa LRA hawapatikani kutoa sababu zilizomlazimisha Kony kusogeza mbele tarehe ya sherehe,duru za mjini Juba zinasema kuwa huenda ni sababu za ugonjwa.

Hata hivyo serikali ya Uganda pia nalo hilo imelipinga.

Waziri wa masuala ya kikanda amesema kuwa sababu kuu ya kuahirishwa huko ingawa wao LRA hawakuwaambia lakini wao wanajua kuwa Kony yuko jamhuri ya Afrika ya Kati kwa hivyo kutembea kwa mguu kutoka huko na kufika Garamba itachukua mda,ndio maana wameoamba kuahirishwa kwa siku ya kutia saini.

Mazunguzo kati ya Kampala na waasi hao yamekuwa yakiendelea Juba kwa miezi 20 sasa tangu ianze Julai mwaka wa 2006.Mkingamo wa Kony umekuwa kuhusu hati ya kukamatwa yeye na makamanda wake wanne na mahakama ya uhalifu ya kimataifa ya mjini The Hague kwa makosa uahalifu wa kivita.

Wanaiomba serikali kwanza ifute kesi hiyo ndio atie saini.Hilo likiwa halijatatuliwa Kony anasema kuwa hatakuja Juba kutia saini huko bali katika mbuga ya wanyama ikiwa atasaini.

Ujumbe wa serikali ambao ulikuwa unajitayarisha kwenda Juba kwa ajili ya sherehe ya kutia sahihi mkataba wa amani wiki hii ,sasa umeahirisha safari hadi wakati mwingine.