Kiongozi wa upinzani Sudan aachiliwa
5 Machi 2019Maafisa wa Sudan wamemuachia huru kiongozi mwandamizi wa upinzani ambaye alikuwa amekamatwa tangu mwezi Desemba kwa kuhusika na maandamano dhidi ya utawala wa Rais Omar al-Bashir, chama chake kimesema leo.
Omar el-Digier, mkuu wa chama cha upinzani cha Sudanese Congress Party, alikamatwa na kufungwa siku kadhaa baada ya maandamano kuzuka Desemba 19 baada ya uamuzi wa serikali kupandisha bei ya mkate mara tatu zaidi.
Maafisa walianzisha ukandamizaji nchi nzima kuzuwia maandamano wakati yakiongezeka nchi nzima dhidi ya Bashir, aliyeingia madarakani katika mapinduzi yaliyoungwa mkono na wanaharakati wa Kiislamu mwaka 1989.
Lakini watu wengine 40 viongozi wa vyama bado wako gerezani, wakati ambapo kiongozi huyo aliyeachiwa huru amesema kwamba maandamano yataendelea dhidi ya Rais Bashir.