1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kizazi njia panda - awamu ya tatu

5 Februari 2015

Miaka mitatu imepita. Mercy na Trudy, ambao walikuwa wakisomea pamoja Bongo Academy, sasa wamejiunga na chuo kikuu kusomea uandishi wa habari. Kwa kujaribu kufuata ndoto yao hiyo, hata wanatia maisha yao hatarini!

https://p.dw.com/p/1EWDG
CROG Season 3
Picha: DW/W.Haferkamp

Urafiki baina ya Mercy na Trudy unakumbwa na majaribu mengi tu, yote haya ikiwa ni kutokana na Mercy kumwambia Trudy siri yake na kisha habari hizo za siri hatimae anazichapisha gazetini. Hatua hii ya Trudy sio tu anamsaliti Mercy, bali pia kunaiweka mashakani familia nzima ya Mercy, huku nae Trudy baadae akipata malipo kutokana na matendo hayo.

Rafiki yao mpya anayeitwa Tina, pia kwake maisha si rahisi! Analazimika kuugawa muda wake kufanya kazi, mbali na masomo yake - japo kwa usiri mkubwa. Hata hivyo, Tina anashindwa kuificha siri hii na kuifichua kwa rafiki zake. Kwa ujasiri na kwa pamoja, Trudy na Mercy wanashirikiana nae kupambana na uovu na ukatili wa mwajiri wake Tina, baada ya kumuonyesha kadi nyekundu.

Dan amerejea Kisimba kumtafuta Mercy na pia kujaribu kujenga uhusiano na mtoto wake Linda mwenye umri wa miaka mitatu sasa. Hata hivyo, jaribio hilo linapingwa vikali na Mercy, kwa sababu bado anakumbwa na changamoto ya kufanikisha masomo yake akiwa mzazi na pia kutumia muda wake mwingi kujenga uhusiano na mumewe Niki, baada ya Niki kuugua. Je wawili hawa wataweza kujenga maisha yao ya baadae wakiwa pamoja?

Hata hivyo lakini, Dan anaamua kubakia nchini Kisimba na kujaribu kujitafutia riziki kupitia mpango wake wa kuhifadhi mazingira.