1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia kwa wanawake Ufaransa yaanza vizuri

Sekione Kitojo
8 Juni 2019

Wanawake wa  Ufaransa  wamechukua  hatua  ya kwanza  kufuata nyayo za  kombe  la  dunia   kwa  wanaume  wa  nchi  hiyo.Imeicharaza Korea kusini kwa mabao 4-0 katika mchezo wa ufunguzi mjini Paris.

https://p.dw.com/p/3K3gC
FIFA Frauen WM 2019 Eröffnung Frankreich - Südkorea
Picha: Imago Images/DeFodi/A. Gottschalk

 Wendie Renard  akiwa  mchezaji  mrefu  kabisa  katika  mashindano  haya ya kombe  la  dunia  kwa  wanawake yanayofanyika  nchini  Ufaransa, alipachika  mabao  mawili  kwa  kichwa  kupitia  mpira  wa  kona, na kikosi  hicho  cha  Les Bleues  kiliwakndamiza  Korea  ya  kusini jana Ijumaa  kwa  mabao  4-0  katika  tamasha  la  ufunguzi  wa  kombe  la dunia.

FIFA Frauen WM 2019 Eröffnung Frankreich - Südkorea Macron und Infantino
Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa (kulia) na rais wa FIFA Gianni Infantino (kushoto)Picha: Imago Images/J. Huebner

Eugenie Le Sommer  na Amandine Henry pia  walipachika  mabao katika  mchezo  uliofanyika  katika  uwanja  wa  mjini  Paris  wa  Parc des Princes, nyumbani  kwa  klabu  maarufu  ya  mjini  Paris , Üaris Saint-Germain.

Mwanamuziki  nyota  wa  mitindo  ya  Pop Jain alihusika  katika sehemu  ya  burudani  kwa  mashabiki  45,261, walioujaza  uwanja huo , na  rais  wa  Ufaransa  Emmanuel Macron  alikuwa  miongoni mwa  watazamaji  wakiimba  wimbo  wa  taifa "La Marseillaise".

Tulijua  kwamba  utakuwa  usiku  wa  hamasa  kubwa . "Lakini nafikiri  tuliutayarisha  vizuri," Renard  alisema. "Wakati  ukiwa  na zaidi  ya  watu 45,000  wakiimba  wimbo  wa  taifa  wa  Ufaransa, bila  shaka  unakuwezesha  kupambana."

Ufaransa  ni  mwenyeji wa  mashindano  hayo  katika  wakati  ambao timu  za  wanawake  zinaongeza  msukumo  wao  kwa  kutendewa haki  kama  wengine  na  shirikisho  la  kandanda  duniani  FIFA pamoja  na  mashirika  mengine  yanayohusika  na  mchezo  wa kandanda.

FIFA Frauen WM 2019 Eröffnung Frankreich - Südkorea
Sherehe za Ufunguzi katika michezo ya fainali za kombe la dunia la wanawake nchini UfaransaPicha: Imago Images/Xinhua/Z. Huansong

Taifa la kwanza kunyakua vikombe vyote vya dunia

Ufaransa  linajaribu  kuwa  taifa  la  kwanza  kunyakua  mataji  yote ya  wanaume  na  wanawake  katika  kombe  la  dunia katika  wakati mmoja.

Nina  hakika  watu  wanamatarajio, ama  matumaini, na hata  sisi  ni hivyo  hivyo, tungependa  kufuata  katika  nyazo za  timu  ya wanaume  ya  taifa," kocha  wa  Ufaransa Corinne Diancre amesema. "Lakini  kila  kitu  kinahitaji  muda. Tumeshinda  usiku  wa leo , lakini  bado  hatujashinda  kitu. Tunahitaji  kuwa  makini  na kuwa  na  malengo  katika  michezo  sita, na  hapo  ndio  tutaona kile kitakachokuja."

FIFA Frauen WM 2019 Eröffnung Frankreich - Südkorea
Amandine Henry wa Ufaransa akishangiria bao dhidi ya Korea kusiniPicha: picture-alliance/AA/M. Yalcin

Norway  na  Nigeria  zinakutana  katika  kundi A la  ufunguzi  leo Jumamosi (08.06.2019).

Ufaransa  inakumbana  na  Norway  siku  ya  Jumatano  na  wana miadi  na  Nigeria  Juni  17.

Wigo  wa  ushindi  wa  Ufaransa  ni  mkubwa  katika  mchezo  wa ufunguzi  wa  mashindano  ya  kombe  la  dunia  la  wanawake  tangu pale  China  ilipoishinda  Norway  kwa  kiwango  hicho  hicho  cha mabao  katika  mashindano  ya  kwanza  mwaka  1991.

Miaka  minne  iliyopita, timu  zote  tisa  ambazo  zilishinda  michezo yake  ya  ufunguzi  zilifika  kutoka  katika  timu  24  za  awamu  ya makundi  hadi  katika  duru  ya  timu  16  bora.

FIFA Frauen WM 2019 Eröffnung Frankreich - Südkorea
Kikosi cha Ufaransa kikishangilia bao katika mchezo wa kombe la duniaPicha: picture-alliance/dpa/R. Sellers

Timu  ya  nne  kwa  ubora  duniani  haikusumbuliwa   kabisa  na namba  14  duniani  ya  Korea  kusini. Ufaransa  ilikuwa imevurumusha mikwaju  17 -0 katika  kipindi  cha  kwanza na ikatandika  mashuti   21-4 kwa  jumla  katika  mchezo  mzima. Hii  ina maana  Korea  kusini  ilielekeza  mikwaju 4 tu  langoni  mwa Ufaransa  katika  mchezo  wote  jana  usiku.

Jioni ya  leo (08.06.2019) timu  ya  Ujerumani itafungua  dimba  la  kundi B kwa kupambana  na  China , na  kisha  Uhispania  itakwaana  na  Afrika kusini.