1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la shirikisho; Leverkusen chali

13 Februari 2014

Katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho , DFB Pokal, timu nne zimefanikiwa kuingia duru ya nusu fainali. Timu hizo ni Borussia Dortmund, Bayern Munich, Kaiserslautern na Wolfsburg.

https://p.dw.com/p/1B816
DFB-Pokal Viertelfinale Bayer 04 Leverkusen 1. FC Kaiserslautern
Mchezaji wa Bayer Leverkusen Sydney Sam akiugulia maumivuPicha: picture-alliance/dpa

Jana timu ya daraja la pili ya Kaiserslautern iliiondoa Bayer Leverkusen katika kinyang'anyiro cha kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal katika mchezo wa robo fainali, baada ya kushinda kwa bao 1-0 katika mchezo ambao ulichezwa kwa muda wa dakika 120 baada ya timu hizo kutoka sare bila kufungana katika muda wa kawaida.

DFB-Pokal Viertelfinale Bayer 04 Leverkusen 1. FC Kaiserslautern
Wachezaji wa Kaiserslautern wakishangiria ushindiPicha: Getty Images

Wolfsburg iliishinda nguvu Hoffenheim kwa mabao 3-2 na Bayern Munich ilidhihirisha ubabe wake kwa kuishinda Hamburg kwa mabao 5-0.

Timu nne Wolfsburg, Kaiserslautern, na Bayern Munich zimeingia nusu fainali ambapo Borussia Dortmund ilikuwa timu ya kwanza kukata tikiti yake kwa kuishinda Eintracht Frankfurt kwa bao 1-0 siku ya Jumanne.