1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yakosoa matamshi ya Blinken juu ya Urusi

Lilian Mtono
11 Novemba 2023

Korea Kaskazini imekosoa matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kuhusiana na uhusiano wake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4YgrI
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipozuru Urusi Septemba, 2023, ziara iliyokosolewa vikali na mataifa ya magharibi
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alipozuru Urusi Septemba, 2023, ziara iliyokosolewa vikali na mataifa ya magharibiPicha: Yonhap/picture alliance

Kulingana na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini, KNCA, Wizara ya Mambo ya Nje ya taifa hilo imeitaka Marekani kukubaliana na uhalisia huo mpya wa uhusiano wao na Urusi.

Imeongeza kuwa haitajali kinachozungumzwa juu yao na kusema uhusiano huo unalenga kuhamasisha amani na kwamba utazidi kuimarika. 

Blinken alisema siku ya Alhamisi kwamba anaunga na Korea Kusini kuonyesha wasiwasi kuhusiana na kuimarika kwa ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Urusi.