1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Korea Kusini huenda ikarejea kwenye nishati ya nyuklia

Saumu Mwasimba
16 Januari 2023

Rais Yoon Suk Yeol wa Korea Kusini amesema juhudi za nchi yake za kuondokana na hewa ukaa kufikia mwaka 2050 zitategemea kwa sehemu kurudi kwenye umeme wa Nyuklia.

https://p.dw.com/p/4MEbf
Südkoreas Präsident Yoon Suk-yeol
Picha: Daewoung Kim/REUTERS

Rais Yoon Suk Yeol amesema juhudi hizo kufikia mwaka 2050 zitategemea kwa sehemu kurudi kwenye umeme wa Nyuklia japo mtangulizi wake alijaribu  kuondokana na nishati ya atomiki. Rais Yoon akizungumza katika mkutano wa kilele katika Umoja wa Falme za Kiarabu amesema ikiwa mataifa hayo yataunganisha juhudi zao katika kuendeleza nishati isiyoharibu mazingira, hatua hiyo haitoimarisha tu usalama wa nishati wa nchi hizo mbili bali pia itachangia uthabiti wa soko la nishati duniani. Umoja wa Falme za Kiarabu pia imeahidi kuondokana na uzalishaji hewa ukaa kufikia mwaka 2050, ahadi ambayo inabakia kuwa ngumu kuifikia na ambayo nchi hiyo ya kiarabu bado haijafafanua ni vipi itafikia azma hiyo. Rais wa Korea Kusini yuko katika ziara ya siku nne katika Umoja wa Falme za Kiarabu pamoja na viongozi wa makampuni makubwa.