1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKosovo

Kosovo yafunga mpaka wake na Serbia kufuatia maandamano

28 Desemba 2022

Kosovo imetangaza kuwa imeufunga mpaka mkubwa zaidi baina yake na Serbia baada ya waandamanaji wa Kiserbia kuzuia barabara upande wa pili wa mpaka wakiwaunga mkono jamaa zao wanaoishi Kosovo kuukataa uhuru wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4LUGi
Mitrovica | Kosovo
Picha: Bojan Slavkovic/picture allliance/dpa

Serikali ya Kosovo ambayo zamani ilikuwa jimbo la Serbia ilijitangazia uhuru wake mwaka 2008, lakini Serbia imekuwa ikikataa kuutambua uhuru huo, na imekuwa ikiwahamasisha Waserbia wapatao 120,000 waishio ndani ya Kosovo kupinga mamlaka ya nchi hiyo mpya.

Maandamano ya hivi  karibuni yalifanyika saa chache baada ya Serbia kutangaza kuwa majeshi ya nchi hiyo yamewekwa katika kiwango cha juu kabisa cha tahadhari wakati mivutano ikishamiri kati ya Belgrade na Pristina.

Sehemu nyingine mbili za mpaka baina ya mataifa hayo zimefungwa kufuatia maandamano yaliyoanza Desemba 10 mwaka huu.