1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kremlin yaitaja operesheni yake nchini Ukraine kuwa ni vita

Tatu Karema
22 Machi 2024

Zaidi ya miaka miwili baada ya Urusi kufanya uvamizi kamili wa kijeshi nchini Ukraine, msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema hatua hiyo sasa ni vita vilivyochochewa na mataifa ya Magharibi.

https://p.dw.com/p/4e26f
Ukraine Kharkiv
Mashambulizi ya Urusi mjini KharkivPicha: Sergey Bobok/AFP

Zaidi ya miaka miwili baada ya Urusi kufanya uvamizi kamili wa kijeshi nchini Ukraine, msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema hatua hiyo sasa ni vita vilivyochochewa na mataifa ya Magharibi.

Vita vya Urusi na Ukraine vimeingia mwaka wa tatu sasa

Katika mahojiano yaliochapishwa leo kwenye jarida la  Argumenty i Fakty, Peskov ameeleza kuwa vita hivyo vilianza kama operesheni maalumu ya kijeshi lakini wakati mataifa ya Magharibi yalipoingilia kati na kulemea upande wa Ukraine, iligeuka kuwa vita kwa taifa hilo.

Hadi kufikia sasa, ikulu ya Kremlin ilikuwa imesisitiza kuwa mashambulizi nchini Ukraine yalikuwa operesheni ya kijeshi iliyolenga kuhakikisha usitishaji wa shughuli za kijeshi na kupinga itikadi za kinazi nchini humo. Hii ilimaanisha kuwa operesheni hiyo ilikuwa ni ya muda tu wakati matumizi ya neno ''vita'' yakipigwa marufuku.

Kwa kujibu swali kutoka kwa vyombo vya habari, Peskov alifafanua kwamba Urusi iko vitani, lakini operesheni hizo za kijeshi bado zitadumisha hadhi yake ya sasa ya kisheria.