1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kufuatia uchaguzi wa Juni ishirini na saba nchini Zimbabwe, Jumuiya ya mandeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika yapeleka waangalizi nchini humo.

Scholastica Mazula12 Juni 2008

Zaidi ya waangalizi miamoja kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika-SADC, tayari wameanza kupelekwa nchini Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/EIUb
Kiongozi wa chama Kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change-MDS, Morgan TsvangiraiPicha: AP

Waangalizi hao wanakwenda kwa ajili ya kusimamia duru ya pili ya Uchaguzi wa urais itakayofanyika nchini humo Juni ishirini na saba.

Wakati huo huo Afisa wa Ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kwenda nchini Zimbabwe wiki ijayo kwa ajili ya kujadili hali ya kisiasa nchini humo na uchaguzi ujao.

Kupelekwa kwa wajumbe hao wa SADC nchini Zimbabwe kumekuja huku Chama tawala cha ZANU-PF chini rais Robert Mugabe wa nchi hiyo kikisema kuwa kitaongeza zaidi wakongwe wa Vita-Maveterani, kwa ajili ya kusaidia kampeni katika maeneo yenye wafuasi wengi wa chama kikuu cha Upinzani cha Movement for Democratic Change-MDC.

Mkurugenzi wa Sekretarieti ya SADC inayohusika na masuala ya kisiasa, ulinzi na usalama, Thanki Mothae, amewaambia waandishi wa habari mjini harare kwamba wako tayari kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.

Mothae, amesema kwamba kiasi cha waangalizi miamoja na ishirini wamepelekwa katika sehemu mbalimbali za nchi, hii ikiwa ni awamu ya kwanza lakini wanatarajiwa kutuma waangalizi zaidi ya mianne ambao watakuwa katika maeneo ya kupigia kura.

Ama kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amemtuma afisa mmoja wa ngazi ya juu katika Umoja huo, Haile Menkerios, kwenda nchini Zimbabwe wiki ijayo kwa muda wa siku tano kwa ajili ya kulisaidia taifa hilo linalojiandaa na duru ya pili ya uchaguzi wa uraisi hapo Juni ishirini na saba.

Menkerio, anatarajiwa kwenda nchini Zimbabwe kuanzia Juni kumi na sita hadi juni ishirini, ambako atafanya mazungumzo juu ya hali ya kisiasa na uchaguzi ujao.

Katika Mkutano kuhusu chakula uliofanyika mjini Roma mapema mwezi huu, Ban Ki-Moon, alikutana na rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na aka ahidi kumtuma Menkerios ambaye ni katibu msaidizi wa masuala ya mahusiano ya kisiasa katika Umoja huo na ndiye mwenye jukumu la kushughulikia masuala ya Kisiasa ya Afrika.

Hivi karibuni rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki alionya juu ya ongezeko la machafuko ya kisiasa nchini Zimbabwe wakati wakielekea katika Duru ya pili ya Uchaguzi.

Mbeki ambaye ni mshauri mkuu wa masuala ya kiasiasa nchini humo, ambapo Morgani Tsvangirai anamatumaini ya kumuondoa madarakani Rais Mugabe.

Kampeni za duru ya pili ya uchaguzi za Tsvangirai, zimesongwa na matatizo mbalimbali kutoka kwenye serikali ya Zimbabwe na tayari katika kipindi cha wiki iliyopita alikuwa ameshikiliwa na polisi mara mbili.

Wakati huo huo, Tsvangirai, ameekishutumu chama Tawala cha ZANU-PF, kwakusambaza mashambulizi kwa wafuasi wa chama cha MDC, lakini anasema anajiamini kuwa atashinda katika uchaguzi wa Juni ishirini na saba baada ya kumshinda rais Mugabe katika duru ya kwanza ya uchaguzi.