1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya kimataifa ya mauaji ya Wayahudi ya Holocaust

Sekione Kitojo
27 Januari 2019

Kila mwaka mwezi Januari, maafisa wa Ujerumani hukumbuka mauaji ya mamilioni ya Wayahudi na makundi mengine ya watu yaliyofanywa na utawala wa Wanazi. Kwa sasa, watu wanajadili,njia "sahihi" ya kukumbuka tukio hilo.

https://p.dw.com/p/3CGkv
Deutschland Bundeskanzlerin Angela Merkel im ehemaligen KZ Dachau
Picha: picture-alliance/AP Photo/K. Joensson

"Wale ambao  hawakumbuki yazamani  wanaweza  kuyarudia." Nukuu  hiyo  ya  mwanafalsafa Mhispania - Mmarekani  na mwandishi George Santayana  inaweza  kuonekana  katika  kambi ya  mateso ya  Auschwitz. Kukumbuka  mauaji  dhidi  ya  Wayahudi, Holocaust kimsingi  imekuwa  juhudi  za  taifa la  Ujerumani  kwa miaka mingi , kutoka  kwa  maafisa  hadi  wabunge. Mvuto  kutoka kwa  umma bado  uko  imara pia. Makambi  ya  zamani  ya  mateso pamoja  na  maeneo  mengine  ya  kumbukumbu  yanapata watu wengi  wanaoyatembelea.

Projekt "Dimensions in Testimony" im Jewish Heritage Museum
Picha za kumbukumbu katika makumbusho ya Wayahudi nchini Ujerumani Picha: picture-alliance/AP Photo/B. Matthews

Na bado, mashirika  ya  Wayahudi  yanasema  yameshuhudia ongezeko  la  chuki  dhidi  ya  Wayahudi  nchini  Ujerumani. "Bingwa wa  dunia  wa kumbukumbu  anapoteza  vita  dhidi ya  chuki za  hivi sasa  dhidi  ya  Wayahudi," anasema Meron Mendel, mkurugenzi wa kituo  cha  elimu  mjini  Frankfurt  cha  Anne Frank. Wasi  wasi  huo unaungwa  mkono  na  uchunguzi  uliofanyika  hivi  karibuni  na shirika  la  Umoja  wa  Ulaya  kwa  ajili  ya  haki  za  msingi  katika mataifa  12  ya  Ulaya. Uchunguzi  huo  umegundua  kwamba  katika mwaka  uliopita, Wayahudi  nchini  Ujerumani  hawakukabiliana  tu na  uhasama  zaidi  kuliko  mwaka  uliopita, lakini  pia  wamekabiliwa na  uhasama  huo  kuliko  katika  nchi  nyingine.

Kiasi  ya  asilimia  41  ya  Wayahudi  nchini  Ujerumani  wamesema walikuwa  wahanga  wa  uhasama  na  chuki  dhidi  ya  wayahudi, ikilinganishwa  na  wastani  wa  asilimia  28 katika  mataifa  mengine yaliyofanyiwa  uchunguzi.

Wasi wasi kwa  Wayahudi 

Kile  kinachowatia  wasiwasi  zaidi  Wayahudi  nchini  Ujerumani ni matamko  yanayotolewa  na  wanasiasa  kutoka  chama cha  siasa kali  za  mrengo  wa  kulia  cha  Alternative for Germany AfD. Mwaka jana, kiongozi  wa  chama  hicho Alexander Gauland  alisema kwamba " Hitler  na  Wanazi  ni tone  tu  la  kinyesi  cha  ndege katika  zaidi  ya  miaka elfu  ya  mafanikio  katika  historia  ya Ujerumani."

Deutschland AfD - Europawahlversammlung in Riesa | Alexander Gauland
Kiongozi wa chama cha AfD Alexander GaulandPicha: picture-alliance/dpa/M. Skolimowska

Na miaka  miwili  iliyopita  kiongozi  wa  AfD  wa  jimbo  la Thuringia Bjoern Hoecke  alitoa  wito  wa  "kubadilika kwa digrii 180" katika  utamaduni  wa  Ujerumani, kwa  kuangalia "hasira" ambazo Gauland  na  Hoecke  walizosababisha. Waziri wa  mambo  ya kigeni  wa  Ujerumani Heiko Maas ametoa  wito kwa  mtazamo  mpya katika  kuwafundisha  watu  juu  ya  Holocaust.

"Kile  tunachohitaji  hivi  sasa  ni mtazamo  mpya  wa  kuadhimisha matukio  ya  kihistoria kwa  manufaa  ya  hivi  sasa," Maas  aliandika katika  makala kama  mwandishi  mwalikwa  katika  gazeti  la kihafidhina  la  Welt am Sonntag ikiingiliana  na  siku  ya  kimataifa ya  kumbukumbu  ya  Holocaust  leo  Jumapili (27.01.2019).

Usiku wa vioo

Amesema  kuwa  kusonga  mbele, historia  inapaswa  kuangaliwa sio tu kama  suala  la  kukumbuka  matukio  yaliyopita lakini  pia kama  suala  la  kuyaelewa matukio  hayo.

Mwanasiasa  huyo  kutoka  chama  cha  SPD  alikiri kwamba  enzi za Wanazi na  mauaji ya Holocaust yanatupwa  kando  kila  muda unavyokwenda.  "Kwa  mtu  aliyezaliwa  leo, "Usiku  wa vioo vilivyovunjika" mwaka  1938 ni  muda  mrefu  sana  kama  utawala wa  kansela  Bismark mwaka 1971 nilipozaliwa. Hii  inabadilisha  jinsi matukio  kama  hayo  yanavyokumbukwa.

New York Außenminister Maas im UN-Sicherheitsrat
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko MaasPicha: picture-alliance/dpa/B. von Jutrczenka

Masinagogi na biashara   zilizokuwa  zinamilikiwa  na  Wayahudi nchini  Ujerumani  ziliporwa  na  kuchomwa  moto  Novemba  9, 1938, siku  ambayo ilikuja  kufahamika  kama "usiku  wa  kuvunjika vioo."

Siku  ya  kimataifa  ya  Holocaust  ni  kumbukumbu  ya  kuuwawa Wayahudi  wa  Ulaya  milioni  6  na  wote  waliouwawa   katika kambi za  mauaji  za  enzi  za  Wanazi. Vikosi  vya  jeshi  la iliyokuwa  Umoja  wa  Kisovieti  vilikomboa kambi  ya  mateso  ya Auschwitz  Januari 27, 1945.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Bruce Amani