1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kumbukumbu ya miaka 25 ya shambulio la chuki dhidi ya wageni

Sekione Kitojo
30 Mei 2018

Magazeti ya Ujerumani yamejishughulisha na mada ya kumbukumbu ya miaka 25 tangu shambulio la chuki dhidi ya wageni nchini Ujerumani,kashfa kuhusu idara ya uhamiaji mjini Bremen, na mzozo wa kuunda serikali nchini Italia.

https://p.dw.com/p/2ybY7
Deutschland Jahrestag 25 Jahre Solinger Brandanschlag | Angela Merkel, Mevluede Genc, Armin Laschet und Mevlut Cavusoglu
Picha: picture-alliance/CITYPRESS 24

Mhariri  wa  gazeti  la  Hannoversche Allgemeine Zeitung akizungumzia  kuhusu  kumbukumbu  ya  shambulio la  kuchomwa moto  nyumba  ya  Bibi  Mevluede Genc raia  wa  Ujerumani mwenye  asili  ya  Uturuki  mjini  Solingen  anaandika:

"Mwaka 1993  bibi Mevluede Genc mwenye  asili  ya  Uturuki alipoteza  watoto wake wawili  wa  kike , wajukuu  wawili  na  mpwa wake  kutokana  na  shambulio  la  kuchomwa  moto  nyumba  yake. Mtu  anaweza  kuelewa  iwapo  mtu  kama  huyu  anaweza  kuishi maisha  yake  yote  akiwa  na  chuki. Mevluede Genc  lakini  alibakia muwazi  kwa  pande  zote na  kuendelea  kuwa   mjenzi  wa  daraja la  maelewano.  Kila  mmoja  iwe  katika  sehemu  ya  mauzo ama katika  ofisi  ya  serikali  tunapaswa  kutafakari  na  kumwangalia bibi Mevluede Genc  kama  mfano. Bibi  huyu  kizee ambae  hana majivuno, mpole ametufunza  unyenyekevu  na  maridhiano."

Deutschland Jahrestag 25 Jahre Solinger Brandanschlag | Mevlüde Genc, Angehörige von Opfern
Bibi Mevlude GencPicha: picture-alliance/dpa/O. Berg

Mhariri  wa  gazeti  la  Leipziger  Volkszeitung   kuhusiana  na  tukio hilo  la  kumbukumbu  mjini  Solingen  anaandika  kwamba  historia ya  maisha  ya  bibi  huyu  inamuacha  mtu  mdomo  wazi.  Mhariri anaendelea:

"Jana  katika  kumbukumbu  ya  miaka  25  bibi  huyu mwenye  umri wa  miaka  75, baada  ya  kuuwawaa kwa watoto  wake,  bado anazungumzoa  kuhusu  maridhiano  na  kusameheana. Hili  si  jambo rahisi  sana."

Gazeti  la  Neue Osnabrücker  Zeitung linaandika  kuhusu  kashfa inayoikumba  idara  ya  uhamiaji  ya  mjini  Bremen  kwa  kuidhinisha maombi  kiholela  ya  wahamiaji  wanaoomba  hifadhi. Mhariri anaandika.

"Tukiangalia  shutuma  za  baraza  la  wafanyakazi  dhidi  ya  idara  ya uhamiaji  na  wakimbizi  ya  Ujerumani, utaona  kwamba  makosa  ya ofisi  hiyo  ya  uhamiaji  mjini  Bremen  ni  tone  tu  katika  bahari. Baada  ya  hapo  utaona  kwamba   viwango  vya  utendaji  kupitia miongozo  ya  kulazimishwa , maombi  hayo  ya  wakimbizi yalifanyiwa  kazi  kwa  juu  juu  tu, bila  ya  kufanyiwa  uchunguzi  wa kina. Kwa  mujibu  wa  hatua  za  haraka ili  kutimiza  sheria  za kikatiba. Pamoja  na  hayo  anapitisha  mtu  huyo  aliyeamua ambaye  ni  mfanyakazi  anayeifanya  kazi  hiyo  bila  ya  kuwa  na ujuzi  unaohitajika."

"Mkuu  wa  zamani  wa  idara  hiyo  Frank-Juergen Weise  aliomba ofisi  ya  kansela  kuweka  mfumo  wa  kuchunguza utaratibu  kazi hizo, baada  ya  kauli  mbiu  maarufu  ya  kansela  ya , tutaweza.  Ni maeneo  mangapi  yameathirika, maelfu  ama  maelfu  kadhaa."

Kuhusiana  na  mzozo  wa  kuunda  serikali  nchini  Italia , gazeti  la Mittelbayerische Zeitung  la  mjini  Regensburg  linaandika.

"Tofauti  na  jinsi Umoja  wa  Ulaya  unavyofanya  mahusiano  yake na  sera  za  kizalendo  za  siasa kali  za  mrengo  wa  kulia  za  rais wa  Marekani  Donald Trump , hatima  hiyo  inaikumba   nchi  jirani yetu  ya  Italia  moja  kwa  moja. Mzizi  wa  fitina  hapa  ni  wasi  wasi wa  kujitoa  kwa  Italia  nchi  yenye  uchumi  wa  tatu  mkubwa barani  Ulaya  kutoka  katika  sarafu  ya  euro  ama  masoko  ya hisa  yanavyoliangalia  suala  la  deni  la  Italia  na  uwezekano  wa kulipa  deni  hilo  la  taifa. Pamoja  na  hayo  kuna  athari  ya  moja kwa  moja  katika  uchumi  wa  bara  lote  la  Ulaya.  Mzozo  huo hata  hivyo  unaweza  kutumika  kama  fursa  kwa  Italia  na  Umoja wa  Ulaya."

Ni  maoni  ya  wahariri  wa  magazeti  ya  Ujerumani , kama yalivyokusanywa  leo  na  Sekione  Kitojo.

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Grace Patricia Kabogo