1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCuba

Kundi la G77+China lataka mageuzi mfumo wa ulimwengu

16 Septemba 2023

Kundi linaloundwa na mataifa yanayoendelea la G77 pamoja na China limeanza mkutano wake wa kilele nchini Cuba kwa kutoa mwito wa kubadilishwa kwa utaratibu unaoongoza mfumo wa dunia.

https://p.dw.com/p/4WQLV
Mkutano wa G77 nchini Cuba
Mkutano wa G77+ China unafanyika nchini Cuba Picha: Esteban Collazo/telam/dpa/picture alliance

Mkutano huo unafanyika katikati mparaganyiko wa mfumo unaoongozwa na mataifa ya magharibi ambayo yanatofautiana kuhusu vita vya Urusi nchini Ukraine, mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na mfumo wa uchumi duniani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel amesema hadi sasa, mataifa tajiri yamekuwa yakiuratibu ulimwengu kwa kufuata maslahi yao na sasa ni juu ya nchi zinazoendelea kubadili mfumo huo. Diaz amesema, nchi zinazoendelea zimekuwa waathirika wa kubwa wa mizozo duniani.

Kati ya wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na takriban wakuu 30 wa nchi na serikali kutoka Afrika, Asia na Amerika ya Kati.