1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuteuliwa Biden

Hamidou, Oumilkher25 Agosti 2008

Wahariri wachambua uamuzi wa Obama kumteuwa Biden kama naibu wake

https://p.dw.com/p/F4N2
Barack Obama na Joe BidenPicha: AP



Mada mbili magazetini hii leo;kuteuliwa Senetor Joseph Biden kuwa naibu wa mgombea wa kiti cha rais kutoka chama cha Democrat Barack Obama na kumalizika michezo ya 29 ya Olympic,jana mjini Beijing.


Tuanze lakini na uamuzi wa mgombea wa kiti cha rais wa Marekani kutoka chama cha Democrat,Barack Obama wa kumteuwa Joseph Biden kama makamo wake wa rais.Gazeti la DRESDNER NEUESTEN NACHRICHTEN linaandika:


"Ni uamuzi wa busara kabisa kumteuwa Joe Biden.Kinyume na Obama ,senetor huyo mwenye umri wa miaka 65 ana maarifa ya kutosha linapohusika suala la siasa ya nje.Na kwa kua anatokana na familia ya wafanyakazi,anaweza kuwavutia wale wapiga kura ambao hadi sasa wamekua wakimuangalia Obama kwa jicho la wasi wasi.Warepublican lakini hawataacha kuitumia hoja iliyowahi kutolewa na Biden aliposema wakati mmoja "Obama hajapevuka vya kutosha kuweza kuwa rais".Watu wanajiuliza pia jinsi Obama anavyopanga kueneza risala yake ya "mageuzi" miongoni mwa jamii.Seuze tena Senetor Biden daima amekua akiangaliwa kama muakilishi wa wenye usemi wa kisiasa mjini Washington.



Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linahisi Barack Obama hakufanya makosa kwa kumteuwa Joe Biden,lakini..........



"Warepublican hawataacha kuutumia uamuzi huo na kuutafsiri kua ni sawa na udhaifu.Kimsingi makosa aliyofanya ni mengine kabisa.Amebuni mpango madhubuti wa nishati,lakini wananchi wanahisi hazingatii hofu zao kuhusu bei ya sasa ya mafuta.Na amekwenda likizo,katika wakati ambapo angeweza kuutumia mzozo wa Caucasus katika kampeni ya uchaguzi wa Marekani,kudhihirisha kipeo chake cha kukabiliana na mitihani.Yeye peke yake ndie anaeweza kusawazisha makosa hayo.Katika mkutano mkuu wa chama cha Democrats huko Denver,Biden pia ataruhusiwa kuhutubia.Lakini macho ya kila mmoja atakodolewa  Obama tuu."


Gazeti la RHIENISCHE POST la mjini Düsseldorf liunaandika:


"Sio namna ya kuachana na mtindo wa kisiasa iliyoendelea hadi wakati huu mjini Washington.Ni ushahidi,hana moyo wa kuleta mageuzi ya kina.Uamuzi wake unamfanya asiaminike.Hawezi kudai kwamba McCain hafai kwasababu ya umri wake ,halafu wakati huo huo anampandisha jukwaani katika kambi yake mwenyewe,mtu aliyejaa mvi kichwani."


Die NEUEN OSNABRÜCKER ZEITUNG linachambua:


"Barack Obama kafanya vyema kumchagua Joe Biden.Uamuzi wake unaeleweka lakini hautasaidia pakubwa .Kwasababu licha ya mizozo yote inayoitikisa dunia,kampeni ya uchaguzi itaamuliwa kwa  masuala ya ndani na sera za kiuchumi .Na hapo Biden hana la ziada.Katika mkutano mkuu wa chame chake atalazimika  Obama atamke kampeni ya aina gani anapania kufuata.Mbinu za kuchomoa wazee hazitoshi."