1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LEVI: Kikosi cha Umoja wa Ulaya kuondoka Kongo Novemba 30

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6i

Ujerumani imesema kikosi cha Umoja wa Ulaya inachokiongoza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kinatakiwa kuondoka nchini humo mnamo Novemba 30 kama ilivyopangwa, licha ya shinikizo la kuwataka wanajeshi waendelee kubakia kuzuia machafuko na kuhakikisha usalama baada ya duru ya pili ya uchaguzi.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani, Franz Josef Jung, amesema katika mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa Umoja wa Ulaya mjini Levi nchini Finland, kwamba anafikiri ni muhimu kuzingatia tarehe 30 Novemba, lakini hakutaka kusema ikiwa matatizo mapya yatatarajiwa.

Hata hivyo Ufaransa, ambayo ina idadi kubwa ya wanajeshi katika kikosi hicho, imesema huenda ikubali kurefusha muda huo kwa mwezi mmoja ikiwa Umoja wa Mataifa utawasilisha ombi katika azimio jipya.

Kikosi cha Umoja wa Ulaya kimepangwa kuondoka Kongo baada ya matokeo rasmi ya duru ya pili ya uchaguzi kutangazwa mnamo Oktoba 29. Inahofiwa huenda kukazuka machafuko baada ya uchaguzi huo.