1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Libya na Marekani uhasama umekwisha.

4 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CkEv

Washington. Waziri wa mambo ya kigeni wa Libya ametangaza kuwa mvutano na Marekani umemalizika rasmi wakati akifanya ziara mjini Washington , kufanywa na mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Libya yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya mahasimu hao wa zamani.

Mohammed Abdel-Rahman Shalgam alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice katika ziara ambayo imegubikwa na hali ya kutoridhika na haki za binadamu nchini Libya pamoja na masuala ya kisheria ambayo hayajamalizika yanayotokana na shambulio la bomu dhidi ya ndege ya abiria ya Marekani katika eneo la Lockerbie nchini Scotland. Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani Sean McCormark amesema Rice amezusha suala la kukamilishwa kwa matukio ya hapo kabla , haki za binadamu na masuala ya kieneo katika mazungumzo yao ya saa moja na Shalgam.

Wakati huo huo Libya imechukua urais wa baraza la usalama la umoja wa mataifa , ikihitimisha kurejea kwa taifa hilo katika kuheshimika tena kimataifa. Lakini balozi wake amesema kuwa matatizo ya hapo zamani ya Libya chini ya vikwazo vya umoja wa mataifa inaiweka nchi hiyo katika nafasi ngumu wakati ikizungumzia kuhusu kuiwekea vikwazo nchi nyingine.