1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LIMA: Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Lima kuwasili Gaza

4 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdY

Naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Peru, Gonzalo Garcia, alitarajiwa kuwasili katika Ukanda wa Gaza kujaribu kumuokoa mpiga picha wa shirika la habari la Ufaransa, AFP, raia wa Peru, Jaime Razuri, aliyetekwa nyara siku mbili zilizopita.

Garcia atakutana na viongozi wa mamlaka ya Palestina, shirika la AFP na viongozi wa Ufaransa kupanga juhudi za kuachiliwa huru kwa mwandishi habari huyo anayezuiliwa na watekaji nyara huko Gaza.

Razuri mwenye umri wa miaka 50 alitekwa nyara mjini Gaza nje ya ofisi ya shirika la AFP alipokuwa anarudi kutoka kazini akiwa ameandamana na dereva na mkalimani wake.

Kufikia sasa hakuna habari zozote kumhusu wala malengo ya watekaji nyara wanaomzuilia.