1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Loew aonya kuhusu kuwachosha wachezaji

Sekione Kitojo
1 Juni 2017

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew, asema vyama vya soka vinahatari kuwachosha wachezaji kwa kuwatumia katika michezo mingi

https://p.dw.com/p/2dzXG
Fußball | Deutschland vs Nordirland | Jogi Löw
Joachim Loew kocha mkuu wa UjerumaniPicha: picture-alliance/augenklick/S. El-Saqqa

"Ni  mchezo  hatari , hatupaswi  kuvuta  kamba  kwa  nguvu  sana," kocha  mkuu  wa  Ujerumani  alionya  katika  mahojiano yaliyofanyika  leo  Alhamis  na  SID, tawi  la  shirika  la  habari  la Ufaransa AFP.

"Unakuwa  na  hisia  kwamba  vitu  tayari vimepauka  na  orodha  ya timu  zinazocheza  inaonekana  kuwa  ya  furaha."

loew amewaacha  wachezaji  nyota  katika  kikosi  chake  kama Thomas Mueller , Mats Hummels, Toni Kroos, Mesut Ozil , Jerome Boateng , Manuel Neuer  na  sami  Kherdira  kwa  ajili  ya  michuano hiyo  ya  Confederation Cup, inayoanza  Juni  17  na  kumalizikia Julai 2, na  amewaita  wachezaji  wapya  kabisa saba.

WM 2014 Training der deutschen Mannschaft 12.6.2014
Wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani wakifanya mazoweziPicha: picture-alliance/dpa

Kujitayarisha  kwa  ajili  ya  kombe  la  dunia  mwakani, Loew amesema  lengo  lake  kuu  nchini  Urusi  ni kutia  damu  changa katika  kizazi  cha  wachezaji  wake  nyota , na  hakusema  lolote kuhusu  kushinda  katika  mpambano  huo  wa  timu  nane.

Ujerumani  inakutana  na  Chile , Australia  na  Cameroon  katika kundi B wakati  Ureno , inakumbana  na  wenyeji  Urusi , Mexico  na New Zealand  katika  kundi  A.

Loew amewajumuisha  wachezaji  watatu  tu  wa  kikosi  cha  kwanza ambacho  kilishinda  kombe  la  dunia  mwaka  2014  na  bila  kuwa na  walinzi  watatu Matthias Ginter, Shkodran Mustafi na  mchezaji wa  kati Julian Draxler  , ambao walikuwamo  katika  kikosi  cha kwanza  katika  fainali  ya  mjini  Rio de Janeiro.

Akiweza  kuifikisha  timu  ya  Ujerumani  katika  awamu  ya  nusu fainali  ya  kila  michuano  mikubwa  ya  fainali  tangu  mwaka  2006, Loew anaonya  kwamba  mipango  ya  FIFA  na  UEFA kupanua mashindano   makubwa  kunaweza  kusababisha  mzigo  mkubwa kwa  wachezaji  na  vilabu.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe