1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON : Brown kuchaguliwa kuongoza Labour

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoj

Chama cha Labour nchini Uingereza kinakutana kumchaguwa Waziri wa Fedha Gordon Brown kuwa kiongozi wake mpya.

Brown ambaye ni mgombea pekee atachukuwa nafasi ya Tony Blair ambaye amekiongoza chama hicho kwa miaka 13.Brown baadae atakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza hapo Jumatano baada ya kutumikia wadhifa wa waziri wa fedha kwa miaka 10. Anarithi uongozi wa chama na nchi iliogawika kwa maoni kutokana na vita vya Iraq.

Brown amesema kile anachotaka kukifanya akiwa Waziri Mkuu ni kuwajumuisha watu kwenye serikali yake na kujenga muafaka.

Amesema serikali yake itajumuisha kila mtu kutoka fani zote za maisha na kwa wakati huo huo kuonyesha kwamba wanaweza kuongoza kukabiliana na changamoto za usoni.

Brown inabidi sasa awashawishi wapiga kura warudi kwenye chama cha Labour ili kukirudisha chama hicho katika kipindi cha nne madarakani.

Uchaguzi mwengine hautarajiwi kufanyika nchini Uingereza hadi hapo mwaka 2010.