1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Polisi wanachunguza video kupata watuhumiwa.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBms

Polisi wanaangalia video za kamera za ulinzi ili kuwapata watuhumiwa baada ya jaribio la shambulio la bomu katika gari siku ya Ijumaa katika ya jiji la London.

Mkuu wa kikosi cha polisi wa kupambana na ugaidi katika mji huo Peter Clarke amesema kuwa gari mbili aina ya Mercedes zilizohusika zilikuwa zimewekwa mafuta, mitungi ya gesi na misumari na zilikuwa zinahusika na suala hilo.

Polisi wamesema kuwa magari hayo yamekuwa na alama nyingi za ushahidi. Kufuatia tukio la siku ya Jumamosi la kigaidi katika uwanja wa ndege wa Glasgow , waziri mkuu Gordon Brown aliitisha mkutano wa pili maalum wa maafisa wa usalama.

Matukio hayo yanakuja miaka miwili baada ya watu 52 kuuwawa katika mashambulizi ya kigaidi katika mfumo wa usafiri mjini London.