1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Vifo vya watoto vyaweza kuepushwa zaidi

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQ0

Idadi ya watoto wanaofariki kote duniani, imepunguka kwa mara ya kwanza.Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto duniani-UNICEF-watoto wapatao milioni 9.7 walifariki dunia katika mwaka 2005,kabla ya kufika umri wa miaka mitano.Idadi hiyo imepunguka kwa asilimia 24 ikilinganishwa na vifo vya watoto vilivyotokea katika mwaka 1999.

Ripoti ya UNICEF inasema,maendeleo hayo yameweza kupatikana kwa sababu sasa watoto wengi zaidi katika nchi zilizo masikini,wananufaika na hatua za kuokoa maisha kama vile kupatiwa nyongeza za Vitamini-A,vyandarua na chanjo.Hata hivyo mkurugenzi wa UNICEF,Ann Veneman amesema,baadhi kubwa ya vifo bado vinaweza kuepukwa na ametoa mwito kuimarisha juhudi