1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON: Washukiwa sita mahakamani kwa tuhuma za ugaidi, Uingereza.

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTX

Watu sita wamefikishwa mahakamani kutokana na msako uliofanywa juma lililopita kusaka magaidi nchini Uingereza.

Mmoja wa washukiwa hao anakabiliwa na mashtaka yanayohusu mpango wa kumteka nyara na kumuua askari-jeshi mwislamu raia wa Uingereza.

Parviz Khan ameshtakiwa pamoja na wenzake sita kwa misingi ya sheria ya kukabiliana na ugaidi.

Watu tisa walikamatwa kwenye msako huo uliotekelezwa alfajiri mjini Birmingham.

Parviz Khan na wenzake wanne waliwasilishwa kwenye mahakama ya London kisha wakarejeshwa tena rumande.

Mshukiwa wa sita anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo ilhali wengine watatu wameachiliwa bila kushtakiwa.