1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Gordon Brown asema wanajeshi wa Uingereza watabakia Iraq

28 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVH

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesisitiza hapo jana kwamba hawezi kukubali pendekezo la kuwekwa ratiba ya kuwaondoa wanajeshi wa Uingereza nchini Iraq.Brown amesema wanajeshi hao wanakazi muhimu ya kufanya nchini humo.

Aidha amesema wanajeshi hao wataendelea kupambana dhidi ya wanamgambo ili kurudisha hali ya usalama katika taifa hilo na kuwapokeza majukumu vikosi vya usalama vya Iraq.Matamshi ya bwana Blair yalilenga kumjibu kiongozi mmoja wa upinzani Sir Menzies Campbell ambaye aliitaka serikali kubadili sera zake nchini Iraq na Afghanstan akisema idadi ya watu wanaouwawa katika nchi hizo mbili imefika kiwango kisichokubalika.

Tangu uvamizi wa Iraq mwaka 2003 wanajeshi 159 wa Uingereza wameuwawa na wengine 73 wameuwawa Afghanstan tangu mwaka 2001.