1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBelarus

Lukashenko atoa wito wa mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine

Tatu Karema
25 Aprili 2024

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema kuna mkwamo katika mstari wa mbele wa mapambano ya Ukraine na kwamba hali hiyo inaruhusu kuanza kwa mazungumzo ya amani.

https://p.dw.com/p/4fB1e
Rais wa Belarus Alexender Lukashenko (Kushoto) na Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Belarus Alexender Lukashenko (Kushoto) na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Demianchuk/TASS/dpa/picture alliance

Rais Lukashenko amesema masuala yaliyojadiliwa kati ya Urusi na maafisa wa Ukraine nchini Uturuki katika wiki za mwanzo za vita kati ya mataifa hayo mawili, yanaweza kutumika kama mahali pa kuanzia mazungumzo hayo.

TASS pia imemnukuu Lukashenko, mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin,akisema kwamba kunaweza kuwa na ''maangamizi ya dunia'' ikiwa Urusi itatumia silaha za nyuklia kulipiza kisasi kwa vitendo vya mataifa ya Magharibi.

Mara kwa mara, Urusi imekuwa ikionya kwamba uungaji mkono wa mataifa ya Magharibi kwa Ukraine kunayaweka katika mapambano ya moja kwa moja na Urusi na huenda ukachochea mzozo wa nyuklia.