1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA: Kenneth Kaunda alazwa hospitalini

6 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCC7

Aliyekuwa rais wa Zambia Kenneth Kaunda amelazwa hospitalini kufuatia mabadiliko katika shinikizo lake la damu.

Msemaji wa rais huyo wa zamani Duncan Mtonga amefahamisha kuwa Kaunda mwenye umri wa miaka 82 alilazwa katika hospitali ya chuo kikuu mjini Lusaka mapema jana lakini hali yake ni tulivu na anaendelea vyema.

Kenneth Kaunda anatarajiwa kutimiza miaka 83 baadae mwezi huu wa April.