1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luxembourg.Umoja wa Ulaya wataka Iran iwekewe vikwazo.

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1r

Mawaziri wa mambo ya nje wa umoja wa Ulaya, wamezitaka kwa pamoja Korea ya Kaskazini na Iran kuachana na mipango yao ya nyuklia na kurejea katika mazungumzo yaliyoitishwa na jumuiya ya kimataifa.

Mkutano wa mawaziri 25 waliokutana Luxembourg wanatarajia kuipeleka Iran mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwekewa vikwazo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesma.

“Haitoepukika kwamba majadiliano ya baraza la usalama yataendelezwa pakiwa na lengo la kufikia maazimio na hatua ya mwanzo ya vikwazo, lakini tunakubaliana vile vile kwamba hiyo haimaanishi mwisho wa mazungumzo pamoja na Iran“.

Wakati huo huo mawaziri hao wa Umoja wa Ulaya wameunga mkono mapendekezo ya Romania na Bulgaria kujiunga na Umoja huo mwezi January mwakani kuliko ilivyokuwa awali kwamba nchi hizo zisubiri hadi mwaka 2008.