1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafikiano kabla ya Bush kuondoka madarakaní

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQPu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleezza Rice amesema,serikali ya Rais George W.Bush inadhamiria kupata maafikiano kati ya Israel na Wapalestina kabla ya Bush kuondoka madarakani. Akaongezea iwapo mkutano wa amani ya Mashariki ya Kati juma lijalo utafuzu,basi utawasaidia wapatanishi wa Israeli na Wapalestina kufikia ufumbuzi wa kuwepo kwa mataifa mawili.

Kwa upande mwingine,Rais wa Israel Shimon Peres amesema itakuwa vigumu kupata makubaliano ya mwisho ya amani ya mashariki ya Kati kabla ya Bush kuondoka madarakani Januari mwaka 2009.Hata hivyo amesema,mkutano wa juma lijalo utakuwa mwanzo wa majadiliano mapya ya amani.

Marekani imezialika nchi na mashirika 40 kuhudhuria mkutano uliopangwa kufanywa juma lijalo mjini Annapolis,Maryland.