1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Ukraine wamemjibu Papa Francis

Sudi Mnette
11 Machi 2024

Maafisa wa Ukraine na washirika wao wamekosoa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis kwa kusema kwamba Kyiv inapaswa kuwa na "ujasiri" wa kujadili kumalizika kwa vita na Urusi.

https://p.dw.com/p/4dMr5
Vatican City | Baba Mtakatifu Francis wakati wa sala ya Malaika
Papa Francis akisoma ujumbe wake kwenye dirisha lake linalotazamana na Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa sala ya mchana ya Malaika wa Bwana.Picha: Alessandra Tarantino/AP/dpa/picture alliance

Maafisa wa Ukraine na washirika wao wamekosoa Kiongozi wa Kanisa Katoliki, Papa Francis kwa kusema kwamba Kyiv inapaswa kuwa na "ujasiri" wa kujadili kumalizika kwa vita na Urusi, kauli ambayo wengi waliitafsiri kama wito kwa Ukraine kusalimu amri.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ukraine na Poland, mshirika mkubwa wa Kyiv, walilaani matamshi ya Papa. Lakini pia jana, Jumapili hiyo, kiongozi wa moja ya makanisa ya Kikristo nchini Ukraine alisema lazima taifa lijihami na uvamizi wa Urusi ulioanza Februari 24, 2022.

Katika ibada maalumu ya Jana Jumapili PapaFrancis ambae mara zote ameonekana kuchukua msimamo wa kutoegemea upande wowote katika vita vya Ukraine na Urusi alisema anaiombea aman Ukraine.