1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano mjini Pretoria yatake Zuma ajiuzulu

12 Aprili 2017

Maelfu ya watu walikusanyika na kuandamana katika mji mkuu wa Afrika ya Kusini, Pretoria. Maandamano hayo yanamtaka Rais Jacob Zuma anayegubikwa na kashfa za rushwa aachie madaraka.

https://p.dw.com/p/2b7Ez
Waandamana kumpinga Rais Jacob Zuma
Watu wakiandama Afrika ya kusini wakimtaka Zuma ajiuzuluPicha: Reuters/M. Hutchings

Maelfu ya watu walikusanyika leo na kuandamana katika mji mkuu wa Afrika ya Kusini,

Pretoria. Maandamano hayo yanamtaka Rais Jacob Zuma ajiuzulu.

Maandamano ya leo yalioelekea moja kwa moja katika ofisi ya rais, yaliandaliwa na vyama vya upinzani baada ya maandamano mengine yaliyofanyika wiki iliyopita.

Maandamano haya yameandaliwa baada ya Rais Zuma kumfuta kazi waziri wa fedha Pravin Gordhan hatua ambayo ilileta harisa kwa umma juu ya ufisadi wa serikali, ukosefu wa ajira na uchumi unaozorota nchini humo.

Maandamano ya leo yaliongozwa na chama chenye msimano mkali cha wapigania uhuru wa kiuchumi, EFF na kushirikiana na chama cha Democratic Alliance.

"Nimehudhuria kwa sababu nataka Zuma ajiuzulu. Ameiuza nchi. Sitaki awe rais tena," Mavis Madisha, mwanachama wa chama cha EFF mwenye umri wa miaka 37 aliiambia AFP.

Ufutwaji kazi wa waziri wa fedha kumezusha hasira kutoka kwa viongozi wa ngazi ya juu kutoka takwimu za ngazi za juu katika chama tawala cha Afrika National Congress (ANC), ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais, Cyril Ramaphosa.

Wakati huo huo leo ni siku ya kuzaliwa Rais Jacob Zuma. Rais huyo anatimiza miaka 75.

Zuma wakati wake hasa wa kumaliza muda wake kama kiongozi wa chama cha ANC na rais wa Afrika ya kusini ni mwezi Desemba.

Lakini Zuma anaonekana tayari kumpendelea mke wake wa zamani ambaye alikuwa ni mwenyekiti wa kamisheni ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Diamini-Zuma, achukue nafasi yake.

Kuhusu maandamano yaliyofanywa wiki iliyopita rais Zuma alisema kuwa maandamano hayo ni kitendo cha ubaguzi.

Mwandishi : Najma Said

Mhariri: Josephat Charo