1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabadiliko ya hali ya hewa bado ni changamoto ulimwenguni

24 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E5KY

Mawaziri wa mazingira kutoka nchi tajiri kiviwanda za kundi la G8 leo wamenza mkutano wao wa kujaribu kutia msukumo juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Japan nchi mwenyeji wa mkutano huo inamatumaini ya kutumia uwenyekiti wake katika kundi hilo la G8 kutoa mwelekeo wa kuandaa mkataba utakaochukua mahala pa rasimu ya Kyoto kufikia mwishoni mwa mwaka 2009.Mkutano huo wa siku tatu mjini Kobe,unahudhuriwa na mawaziri na maafisa kutoka nchi 8 tajiri duniani pamoja na Brazil,China India,Indonesia,Mexico,Afrika Kusini,na Korea Kusini.Katika kikao cha ufunguzi hii leo Wanaharakati wa mazingira na wafanyibiashara wametopa mwito wa kuchukuliwa hatua za haraka kuweka malengo ya kupunguza viwango vya utoaji gesi chafu ambayo ni chanzo cha ongezeko la ujoto duniani. Mkutano huo unatazamiwa kufungua njia ya kufikiwa makubaliano juu ya mkataba mpya utakaochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto unaomaliza muda wake mwaka 2012.Wanasayansi wa Umoja wa mataifa wameonya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni huenda yakahatarisha maisha ya mamilioni ya watu kufikia mwishoni mwa karne hii.