1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabenki 7 ya Ulaya yako hatarini

Thelma Mwadzaya24 Julai 2010

Mabenki 7 kati ya yote 91 barani Ulaya yameshindwa kuvitimiza vigezo vilivyowekwa kwenye tathmini ya kuhimili misukosuko katika sekta ya fedha.

https://p.dw.com/p/OTfh
Nembo ya benki ya Hypo Real Estate (HRE)Picha: ap

Benki ya serikali ya Hypo Real  Estate  pekee ya hapa Ujerumani ndiyo iliyoingia kwenye orodha hiyo.Benki hiyo ilitaifishwa mwaka 2008.Taasisi nyengine zilizoingia kwenye orodha  hiyo ni benki inayosimamiwa na serikali  ya Ugiriki ya ATE na mabenki mengine matano madogo ya Uhispania.Mabenki  hayo  yameamriwa kuuongeza mtaji wao hadi ufikie kiasi  cha dola bilioni 3.5.Lengo  la tathmini hiyo lilikuwa kuugundua  uwezo  wa mabenki wa kuhimili misukosuko  ya kiuchumi  kadhalika kuwatia imani zaidi  wawekezaji katika eneo la  mataifa  yanayotumia sarafu ya euro. 

EU Finanzminister Luxemburg schäuble rettungsschirm
Mawaziri wa Fedha wa mataifa yanayotumia sarafu ya euroPicha: foto: AP

Hata hivyo bado kuna masuala yaliyojitokeza kuhusu tathmini yenyewe.Shirika la Kimataifa la Fedha ,IMF limeyapongeza matokeo ya tathmini hiyo.Kwa  upande  wake Waziri wa  Fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble ameipongeza hatua hiyo na kuielezea kuwa ya kuimarisha imani  katika masoko ya  fedha.