1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mada mbili kuu zimehanikiza

Oumilkher Hamidou25 Mei 2009

Eti uchaguzi wa rais wa shirikisho ndio njia ya muungano ujao?

https://p.dw.com/p/Hwz7
Kansela Merkel ampongeza rais KöhlerPicha: AP

Mada kuu magazetini hii leo inahusu mkutano mkuu wa kanisa la kiinjili la Ujerumani.Lakini kiini cha uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani ni kuhusu uchaguzi wa rais wa shirikisho.Gazeti la Die Welt linaandika:

"Imetokea kama ilivyokua ikitarajiwa, Horst Köhler ameidhinishwa madarakani.Baraza kuu la wawakilishi halikuzusha maajabu yoyote,na zilzala ya kisiasa ndio kabisa haijashuhudiwa.Aliyekua akishikilia wadhifa huo,amechaguliwa tena-na safari hii -tangu rauni ya kwanza-hata kama haujapindukia wingi unaohitajika.Kwamba uchaguzi umefanyika kama inavyotahiki ,sababu inatokana na Gesine Schwan.Ingawa hilo ni pigo la tatu kwa SPD , kwa kushindwa kwa mara nyengine tena mgombea wao, wamenusurika lakini na ushirika pamoja na wafuasi wa mrengo wa shoto Die Linke na walinzi wa mazingira Die Grüne au ushirika wa nyekundu-nyukendu na kijani.Wasocial Democratic hawajakosea walipotangaza kuwa nyuma ya rais wa shirikisho.Wamemtolea mwito apiganie nidhamu katika shughuli za kiuchumi.Wengi wanasubiri kwa hamu kujua mhula wa pili wa wadhifa wake utakua wa aina gani na nini anapanga kutanguliza mbele.Kwa vyovyote vile awamu hii ya pili inampatia uhuru mkubwa zaidi kuliko ya mwanzo na mwenyewe Köhler anatambua:"

Gazeti la TAGESZEITUNG la mjini Berlin linachambua zaidi kuhusu kushindwa mgombea wa chama cha SPD Gesine Schwan na kuandika :

Hili ni pigo la tatu kwa SPD baada ya Kurt Beck na Andrea Yipsilanti.Kwa mkumbo mmoja imefifia pia ndogo ya kushirikiana pande tatu za nyekundu nyekundu na kijani.Kwanza Gesine Schwan aliwalaumu vikali wafuasi wa mrengo wa kushoto Die Libke kabla ya kulainisha matamshi yake lilipohusika suala la Ujerumani mashariki ya zamani-jambo lililowakasirisha kwa upande wao walinzi wa mazingira Die Grüne.

Gazeti la DER NEUE TAG la Weiden linachambua uchaguzi wa rais wa Shirikisho kwa mtazamo wa uchaguzi mkuu wa September mwaka huu na kuandika:

"Uchaguzi wa Köhler umewaleta pamoja wafuasi wa vyama ndugu cha CDU/CSU na waliberali wa FDP na kuleta mfarakano miongoni mwa wafuasi wa mrengo wa shoto.Lakini kama uchaguzi huo utatosha kweli kubuni muungano wa nyeusi na manjano,hakuna ajuaye.Kwakua hakuna anaetaka kuungana na Die Linke,walinzi wa mazingira nao hawataki mfumo wa Jamaica,yaani Neusi-manjano na kijani na waliberali hawataki muungano pamoja na SPD na walinzi wa mazingira-yadhihirika kana kwamba muungano wa vyama vikuu utaibuka tena uchaguzi utakapomalizika mwisho mwa mwezi wa September.

BdT Kirchentag
Daraja ya kuunganisha waumini wa dini tofautiPicha: AP

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu mkutano mkuu wa kanisa la kiinjili mjini Bremen.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:

Mkutano mkuu huo wa kanisa ni kongamano la wenye kuridhia shingo upande.Si mahala pa kupaza sauti kukosoa ubepari na utandawazi.Kila mmoja anatendewa vyema bila ya kujali anafuata chama gani cha kisiasa-hakuna kulaumiana.Unaepuka mivutano,mamoja,linahusika suala la kisiasa,imani au mdahalo kati ya waumini wa dini tofauti.Mabishano japo kidogo yanahitajika lakini,kwasababu yanasaidia mambo kusonga mbele.

Mwandishi:Oummilkheir Hamidou

Mhariri:Abdul-Rahman