1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waandamana Morocco kupinga mahusiano na Israel

Saumu Mwasimba
12 Februari 2024

Maelfu ya raia wa Moroco waliandamana kwa mara nyingine jana Jumapili kwenye viunga vya mji mkuu, Rabat, kushinikiza nchi hiyo isitishe mahusiano yake na Israel inayoituhumu kwa "mauaji ya halaiki" Gaza.

https://p.dw.com/p/4cIXX
Morocco| Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina
Wamorocco wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kuwaunga mkono WapalestinaPicha: AFP

Waandishi habari wa shirika la AFP wamekadiri zaidi ya watu 10,000 walishiriki mahusiano hayo, wengi wamebeba bendera ya Palestina. Mabango ya waandamanaji yalikuwa na ujumbe unaoesema  "Uhusiano na (Israel) ni Uhaini" na "Komesha mauaji ya halaiki".

Maandamano sawa na hayo yalifanyika kwenye mji mkuu wa kibiashara wa Moroco wa Casablanca Novemba mwaka jana. Tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na kundi la Hamas, maandamano makubwa yamekuwa yakifanyika kwenye taifa hilo la ufalme la Afrika Kaskazini kutaka uhusiano na Israel usitishwe.

Morocco ilirekebisha mahusiano yake na Israel mnamo mwaka 2020 chini mkataba uliosimamiwa na Marekani. Moroco ilinufaika na mkataba huo kwa Marekani kutambua madai yake ya kulimiliki eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.