1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu waathiriwa na mafuriko mashariki mwa Kongo

20 Aprili 2024

Maelfu ya kaya pamoja na miundombinu ya kijamii ikiwemo shule zimeathiriwa na mafuriko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, huku mamlaka likiomba msaada wa haraka kutoka serikali kuu mjini Kinshasa.

https://p.dw.com/p/4f012
Eneo lililoathirika kwa mafuriko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Eneo lililoathirika kwa mafuriko Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: GLODY MURHABAZI/AFP

Msemaji wa mamlaka ya mji wa Uvira Dominique Kalonzo amesema, takriban nyumba 4,500 zimebomoka, zaidi ya viwanja 2,000 vikifunikwa na maji huku zaidi ya kaya 7,000 pamoja na shule 53 zikiathiriwa kutokana na mito iliofurika na kuongezeka kwa kina cha maji ziwa Tanganyika.

Msemaji huyo ameongeza kwamba wakaazi walioathirika wamejihifadhi kwa ndugu na jamaa huku wengine wakilala nje licha ya hali mbaya ya hewa, huku akisisitiza kuwa halmashauri ya mji imeomba msaada wa dharurakwa serikali kuu na mashirika ya kiraia kutokana na mji kukabiliwa na hatari ya kukumbwa na magonjwa.

Soma pia:Burundi yahitaji msaada kukabiliana na mafuriko makubwa

Mbali na Kongo eneo la Afrika mashariki linakumbwa na mvua kubwa iliosababisha vifo vya watu 58 nchini Tanzania katika wiki mbili za kwanza za mwezi Aprili na wengine 32 hivi karibuni nchini Kenya.