1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu wakusanyika kumuunga mkono Chamisa nchini Zimbabwe

22 Agosti 2023

Maelfu ya watu walikusanyika katikati ya mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, kuhudhuria mkutano wa kampeni wa mwanasiasa mkuu wa upinzani Nelson Chamisa.

https://p.dw.com/p/4VRAZ
Mikutano mingi ya Nelson Chamisa ilipigwa marufuku na baadhi ya wafuasi wake walishambuliwa
Mikutano mingi ya Nelson Chamisa ilipigwa marufuku na baadhi ya wafuasi wake walishambuliwaPicha: KB MPOFU/REUTERS

Taifa hilo la kusini mwa Afrika litafanya uchaguzi mkuu wa urais na wabungekesho Jumatano.

Mikutano mingi ya mwanasiasa huyo wa upinzani ilipigwa marufuku na baadhi ya wafuasi wake walishambuliwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanaharakati wa chama tawala cha ZANU-PF.

Chamisa mwenye umri wa miaka 45 anawania urais dhidi ya Rais Emmerson Mnangagwa.

Kura hiyo inatizamwa kwa karibu kama kipimo cha umaarufu wa chama cha ZANU-PF.

Chama hicho kimekuwa madarakani tangu Zimbabwe ilipopata uhuru miaka 43 iliyopita.

Uchumi wa Zimbabwe umegubikwa na mfumuko mkubwa wa bei uliopanda kwa asilimia 175.8 mnamo mwezi Juni na hatimae kupungua mwezi Julai kwa asilimia 101.

Benki ya Dunia inaelezea viwango vikubwa vya madeni visivyo endelevu vinavyoikabili Zimbabwe.