1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya wakulima wakutana Berlin kwa kilele cha maandamano

15 Januari 2024

Msafara mkubwa wa matrekta umemiminika mjini Berlin Jumatatu wakati wakulima wakikusanyika kwa kilele cha wiki ya maandamano.

https://p.dw.com/p/4bF9P
Watu wapatao 10,000 wengi wakiwa ni wakulima wanatarajiwa kuhudhuria.
Watu wapatao 10,000 wengi wakiwa ni wakulima wanatarajiwa kuhudhuria.Picha: Ardan Fuessmann/IMAGO

Maandamano hayo ni ya kupinga mpango wa kuondoa kuondoa ruzuku ya kodi kwenye dizeli wanayotumia.

Polisi ilisema jana kuwa sehemu iliyotengwa kwa ajili ya magari mbele ya Lango maarufu la Brandenburg, ambako maandamano hayo yanafanyika, tayari ilikuwa imejaa.

Katika wiki iliyopita, wakulima walizifunga barabara kuu na kupunguza kasi ya magari kote Ujerumani kufuatia maandamano yao, kwa nia ya kuishinikiza serikali ya Kansela Olaf Scholz kuachana kabisa na mpango wa kuondoa nafuu za kodi kwenye sekta ya kilimo.

Maandamano hayo yaliyoanza Jumatatu iliyopita yameongeza shinikizo kwa serikali ya mseto ya Kansela Sholz ambayo bado inahangaika kutatua mzozo kuhusu bajeti ya mwaka ujao.

Watu wapatao 10,000 wengi wakiwa ni wakulima wanatarajiwa kuhudhuria.