1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafuriko yakwamisha watalii karibu 100 Maasai Mara

Sudi Mnette
2 Mei 2024

Takriban watalii 100 ni miongoni mwa idadi kubwa ya waliokwama baada ya mto kufurika katika hifadhi ya wanyamapori maarufu ya Maasai Mara nchini Kenya kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika maeneo hayo.

https://p.dw.com/p/4fP9M
Kenia | Luftaufnahme überflutetes Maasai Mara Nationalreservat
Mwonekano wa Hifadhi ya Kitaifa ya Maasai Mara iliyofurika, ambayo na kusababisha watalii wakiwa wamekwama katika Kaunti ya Narok, Kenya, Mei 1, 2024.Picha: Bobby Neptune/AP Photo/picture alliance

Afisa mwandamizi katika kaunti ndogo ya Narok Magharibi, Stephen Nakola ameliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP kwamba takriban watalii 100 au zaidi wamekwama katika nyumba za kulala wageni na maeneo ya kuweka kambi ya mbugani.

Hali ilivyo imesababisha pia ugumu wa kuzifikia baadhi ya kambi. Maasai Mara maarufu duniani, iliyo kusini-magharibi mwa Kenya, ni kivutio cha watalii na makazi ya wanyamapori asilia wakiwemo wale wanaojulikana kama "Big Five",  simba, tembo, vifaru, chui na nyati pamoja na twiga, viboko na duma.