1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Mafuriko yaua watu 14 Kenya, familia elfu 15 zaathirika

6 Novemba 2023

Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko nchini Kenya imefikia watu 15 na wengine wakijeruhiwa baada ya kusombwa na mafuriko maeneo mbalimbali nchini humo.

https://p.dw.com/p/4YTI2
Nyumba ikiwa imejaa maji, sehemu ya athari ya mafuriko
Nyumba ikiwa imejaa maji, sehemu ya athari ya mafurikoPicha: Salto City Hall/AFP

Kulingana na shirika la msalaba mwekundu maelfu wameachwa bila makao huku ikikadiria hasara kubwa zaidi mvua hiyo inapoendelea kunyesha. 

Mgogoro wa kibinadamu huenda ukashuhudiwa kutokana na athari za mafuriko yanayoshuhudiwa nchini Kenya hasa maeneo ya pwani, Kaskazini Mashariki, bonde la ufa na magharibi mwa nchi.

Kulingana na shirika la msalaba mwekundu, zaidi ya familia elfu 15 zimeathiriwa, mifugo zaidi ya elfu moja wamefariki, na mazao ya mashamba kiasi cha heka 241 yameharibiwa na mafuriko.

Soma pia:Wokoaji wanapambana kufikia wahanga wa mafuriko India

Mbunge wa Nyandarua Faith Gitau aamesema miongoni mwa madhara yaliosababishwa na mvua hizo ni pamoja na mazao kuoza shambani na miundombinu ya usafiri kuharibika vibaya.

"Tunahitaji watu watathmini waje wakague ili kujua namna gani maji yaha yataelekezwa kwenye mkondo wake." Alisema.

Hali ya miundombinu yatatiza mawasiliano

Mafuriko yamesababisha kukatika kwa madaraja, barabara zikifurika kiasi cha kutopitika na hivyo kutatiza huduma muhimu kama vile uchukuzi wa vyakula, mitihani ya kitaifa inayoendelea, na wagonjwa kufikia vituo vya afya.

Viongozi kutoka maeneo ya kaskazini mashariki wanataka hali hii ya mafuriko itangazwe kuwa janga la kitaifa huku wakiomba msaada wa mahitaji muhimu. 

Fukwe za Ziwa Victoria Siaya-Kenya zakumbwa na mafuriko

Idara ya utabiri wa hewa nchini Kenyaimesema mvua kubwa itaendelea kunyesha ikiandamana na radi kwenye baadhi ya maeneo.

Kuna wasiwasi wa mlipuko wa magonjwa yanayotokana na maji, kufuatia kufurika na kusombwa kwa vyoo.

Soma pia:UNICEF: Majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa yalisababisha watoto milioni 43.1 kupoteza makazi yao kati ya mwaka 2016 hadi 2021

Amos Mariba Kamishna wa kaunti ya Mandera anawahimiza wakaazi kuzingatia usalama wao wakati huu.

Katika baadhi ya maeneo athirika ndege aina ya helikopta zimetumika kuwaokoa watu na kusambaza mitihani kwa watahiniwa wanaoendelea na mitihani ya kitaifa.