1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magaidi wauwana wao kwa wao Nigeria

Saumu Mwasimba
21 Januari 2020

Mapigano makali ya kufyatuliana risasi kati ya makundi mawili ya itikadi kali kaskazini mashariki mwa Nigeria yamesababisha wapiganaji wengi kuuwawa, kwa mujibu wa duru zinazofahamu juu ya tukio hilo. 

https://p.dw.com/p/3WXpC
Symbolbilder Niger Armee
Picha: Getty Images/AFP/I. Sanogo

Wapiganaji waliokuwa kwenye magari ya wazi kutoka tawi la Boko Haram ambalo ni tiifu kwa Abubakar Shekau waliIvamia kambi moja ya kundi hasimu ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu la Afrika Magharibi (ISWAP) na kusababisha makabiliano makali ya risasi ambayo yalisababisha vifo vingi.

Wapiganaji wa Boko Haram waliishambulia kambi ya kijiji cha Sunnawa katika wilaya ya Abadam karibu na mpaka na Niger.

Wanamgambo wa kundi la ISWAP awali waliwavamia Boko Haram katika eneo la Diffa lililoko jirani ya Nigeria ambako waliwateka nyara wanawake 13.