1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: CDU/FDP wanunua data Posta,Uislamu Ujerumani

Sekione Kitojo
3 Aprili 2018

Wahariri magazeti Ujerumani wamejishughulisha na suala la ununuzi wa data za wateja wa shirika la posta na vyama vya CDU na FDP, mjadala wa CDU /FDP kuhusu Uislamu Ujerumani, hali mashariki ya kati Israel na  Palestina.

https://p.dw.com/p/2vP8K
Horst Seehofer - Innenminister - Islam und Deutschland
Picha: picture alliance/dpa/S. Hoppe

 

Tukianza  na  gazeti  la  Der neue Tag  la  mjini  Weiden  kuhusu kuuzwa  kwa  data  za  wateja na shirika  la  posta  kwa  vyama vya CDU na  FDP, mhariri  anaandika.

 

"Ni  kitu  gani shirika  la  posta linafahamu  kuhusu  sisi na kuuza kwa mtu mwingine taarifa  hizo  kwa  fedha. Data kuhusu  uwezo wa kununua, matumizi ya benki, jinsia, umri, elimu, mahali  anakoishi, iwapo ana  familia na iwapo anamiliki  gari. Posta iliuza  data  hizi za raia  kama  ilivyofanya kwa  idara ya  serikali  inayohusika  na magari na ofisi ya  ardhi. Vyama  vilifaidika  na  hilo? anauliza mhariri. Wanaweza  kutumia  data  hizo  kwa  ajili  ya  kuwafikia watu  hao kwa njia  ya  matangazo."

Gazeti  la Stuttgarter nachrichten akizungumzia  suala  hilo  la kuuzwa  kwa  data za  wateja  anaandika:

"Posta  imekuwa  kama  buibui  katika  mtandao  wa  data   nchini Ujerumani. Kila  mtu nchini  Ujerumani  ana  anuani  yake , na inatumbukia  moja  kwa  moja  katika benki  yake ya  data, na  kama unataka  data  hizo ni  lazima uombe kwa  maandishi. Hii  ina  maana gani, inamfanya  mtu  apate  kizungumzu.  Shirika tanzu la  Posta - Deutsch Post Direkt GmbH lina kiasi ya  taarifa  za  binafsi  za watu zaidi  ya  milioni 34   katika  majumba  yapatayo  milioni  24  nchi nzima.  Hii anaandika  mhariri  inaweza  kuifanya  kashfa ya  kuvuja kwa  data  za  watumiaji  wa  mtandao  wa  kijamii  wa  Facebook kuona  wivu. Hii  inaonekana  kuwa  haina  madhara na  ni halali kisheria  lakini  inaonekana  kivingine."

Kuhusiana  na  mjadala  kuhusu Uislamu  nchini  Ujerumani  gazeti  la Rhein-Zeitung  la  mjini  Koblenz  linaandika.

Freitagsgebet - Islam und Debatte
Waumini wa dini ya Kiislamu wakisali nchini UjerumaniPicha: picture alliance/dpa/R. Hirschberger

Kile kinachokera kuhusiana  na  mjadala  huu  juu  ya  Uislamu  ni kwamba  hauna  mwelekeo wowote na  mara kadhaa  ni  kutokana na  matamshi tu ya  kijinga. Kwasababu  mwanasiasa  kama  Horst Seehofer alikuwa  anataka  kusema  nini  kwa  matamshi  yake kwamba "Hakuna uhusiano  kati ya  Uislamu  na  Ujerumani" Kwamba  Uislamu haupaswi tena  kuwapo nchini  Ujerumani ? Kwamba Uislamu  haupaswi kufundishwa  hapa Ujerumani ? Misikiti ifungwe? Waislamu  wote  wanapaswa  waondolewe ?  Mtu anaweza kuzungumzia  hilo  kwa  maneno  mengine.  Hosrt Seehofer  na chama  chake  cha  CSU wanahatarisha  amani  ya  Ujerumani, inasababisha  ugumu  wa  Waislamu  kujumuika  katika  jamii  ya Ujerumani, na  kuongeza  hali  ya usalama na  hatari  zaidi

Gazeti  la  Frankfuerter Rundschau , kuhusiana  na  hali  ya mapambano  kati  ya  Wapalestina  na  Israel  linaandika.

"Katika  ripoti  ya  Umoja  wa  Mataifa  tayari  ilishatolewa  tahadhari, kwamba  kuna  hatari  Gaza  katika  mwaka  2020 itakuwa  sehemu ambayo  haiwezekana  mtu  kuishi. mapambano  yaliyotokea  katika siku  ya  Ijumaa  kuu , wakati  Wapalestina  karibu  30,000 walifanya maandamano  yaliyopewa  jina  la maandamano ya  kurejea walijikusanya  katika  uzio  wa  mpaka na  Israel , na  suala  hilo kuliweka  katika  hali  ya  kuangaziwa  kimataifa. Miito  kwa  pande zote ,  kujizuwia  haisaidii  tena.  Mradi  mahsusi  ya  ujenzi  wa bandari, mifereje  ya  maji  taka  inayofanyakazi, uwezekano wa kuwekwa  nishati  ya  jua  kwa  ajili  ya  umeme haya  yanaweza kupunguza kwa  njia  halisi  msuguano  huo. Mzingiro  mkali  wa eneo  hilo  ni  lazima  ufike  mwisho, ili  watu wa  Gaza  wasipoteze kabisa  matumaini."

Mwandishi: Sekione  Kitojo / inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman