1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini: Uhuru wa vyombo vya habari

Sekione Kitojo
3 Mei 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi leo Alhamis na mada kuhusu siku ya kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, bajeti ya Umoja wa Ulaya pamoja na maadhimisho ya mwaka 200 tangu kuzaliwa Karl Marx.

https://p.dw.com/p/2x6Ee
DW Tag der Pressefreiheit 2018

Gazeti  la  Badische Zeitung  la  mjini  Freiburg  katika  siku  ya  kimataifa  ya uhuru  wa  vyombo  vya habari  linaandika:

Uhuru wa  vyombo  vya  habari unaingia  katika  kila  kitu. Kila  mahali. Ni  haki isiyoweza kuwekwa  katika  mjadala  na  ni  sehemu  ya  uhuru  wa  kutoa maoni  na  demokrasia. Kwanza  kabisa  vyombo  vya  habari  vilivyo  huru vinawezesha  jamii  kuwa  huru. Pale  ambapo  hakuna , kuna  uwezekano kwa  wenye  madaraka  kutumia  hali  hiyo  kufungua milango  ya kutumia vibaya  madaraka  yao. Kuyaona  haya  sio  tu  China  na  Korea  kaskazini.

Hata  nchini  Uturuki  kumekuwa  na  hali  ya  ukandamizaji  dhidi  ya waandishi  habari  na  kubanwa  kwa  haki  za  kiraia. Nchini  Hungary  ama hata  Poland  hali  ya  vyombo  vya  habari  vya  binafsi  ni  mbaya  na vinatakiwa  kufuata  muongozo wa  vyombo  vya  serikali. Katika  hali  hiyo kitisho  cha  uhuru  wa  vyombo  vya  habari  si  tu  kwamba  ni  kikubwa, lakini maafisa, wanajaribu  kuwatumia  waandishi kuandika  kile  wanachotaka  ili kujenga  ukuta, na  kuwatumia  wadau wa habari,   pamoja  na  wagombea  wa kiti  cha  meya na  kuondoa  uhuru wa vyombo  vya  habari  kama tunavyouelewa  leo  hii  na  kuondoa  kuaminika  kwao.

Berlin - Tag der Pressefreiheit 2017 | Schild Reporter ohne Grenzen
Picha: picture-alliance/Eventpress/Stauffenberg

Kuna  dawa  lakini  kwa  hili. Ni  kuwa  wakweli  katika  uandishi  habari. Sio kutofanya  makosa , lakini  kuwa  wakweli  kuhusiana  na mapambano  ya kupata  taarifa  muhimu.

Gazeti  la  Die Welt linaandika  kuhusu  siku  ya  kimataifa  ya  uhuru  wa vyombo  vya  habari. Mhariri  anaandika:

Katika  bahari  ya  dunia  ya  kutovumiliana  na  hali  inayoongezeka  ya kubanwa  kwa  uhuru  wa  raia Ujerumani  ni  kisiwa  kilichobarikiwa.  hata hivyo  ni  lazima  tunalazimika  kuangalia  kwa  kina , kazi  za  waandishi habari  ama vyombo  vya  habari  kwa  ujumla  vinapata vizuwizi  ama kushindwa  kufanya  jambo.

Hii  pia inahusika  katika  mjadala  ambao  hivi sasa  unafanyika  kuhusiana  na  jukumu  la huduma  za utangazaji  halali  kwa umma na  kuna  nafasi  gani  kwa  vyombo  vya  habari vinavyopata  fedha kutoka  vyanzo vya  binafsi katika  uchumi  wa  nchi. Matamanio  makubwa  ya uhuru  nchini  Marekani  ni  muhimu kwa wadau wa  uhuru  wa  vyombo  vya habari  hapa  Ujerumani  kuutilia  maanani.Hakuna  mtu mwenye  uhakika kuhusiana  na  adui  wa  ndani.  Uhuru  wa vyombo  vya  habari  ni  lazima  kila siku uelezewe  upya. Kutokuwa  na  uhuru  ni  hali  bila  shaka  iliyopo  duniani kote, lakini  mara  nyingine  hata  kwetu  hali  hiyo  ipo.

Nalo gazeti la  Frankfurter Allgemeine Zeitung, linazungumzia  sera  ya bajeti , mhariri  anaandika:

Angalia  hesabu, unakosa  kuona, licha  ya  changamoto za wahamiaji, kidigitali, mabadiliko  ya  tabia  nchi  na  uchokozi  duniani  Umoja  wa  Ulaya na  pia  Ujerumani  zinataka  kuyaweka  mambo  hayo  katika  wakati  uliopita.

Licha  ya  kujitoa  Uingereza , nchi  ya  pili  inayochangia katika  bajeti  ya Umoja  huo,  matumizi  ya  Umoja  wa  Ulaya  yanatakiwa  kupanda na  suala la  kilimo  litatamalaki  katika  bajeti  hiyo. Bajeti  ya  Ujerumani  ikiwa  na mtazamo  wa  kijamii  ni  mzigo  kwa  vijana. Nani , kama  sio  wao,  watalipia malipo  ya  uzeeni  ya  ziada  pamoja  na  mambo  mengine  yaliyomo. Chini ya  uongozi  wa  kansela  Angela  Merkel  sera za  kijamii  zinapata  nguvu kuliko  mishahara  ya  wafanyakazi.

Nalo  gazeti  la  Märkische Oderzeitung  la  Frankfurt/Oder  linazungumzia kuhusu  miaka  200  ya  kuzaliwa  kwa  Karl Marx. Mhariri  anaandika:

"Hisia nzuri  hususan kwa  Wajerumani wenye  umri  mkubwa  kutoka iliyokuwa  Ujerumani  mashariki  kwa Marx  haihusiani  na kumbukumbu  ya enzi  ya  DDR. Ni  kuhusu  hamu iliyopo baada  ya  kuwapo  katika  dunia bora  zaidi, kuliko  ahadi ya  malipo. Usoshalisti , uhalisia  wake , kwa  wengi hauwezi  kubadilishwa kama  ulivyofikia mwisho wake. Kwa sababu mapinduzi katika  nchi  ambayo  si  sahihi , nchini  Urusi, yalianzia, wakati mawazo  hayo  yalitumika  vibaya  ama  wakati  haukuwa  sahihi.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman