1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Magazetini

Hamidou, Oumilkher21 Februari 2008

Kashfa ya kodi ya mapato na kashfa ya UNICEF ni miongoni mwa mada zilizochambuliwa magazetini hii leo

https://p.dw.com/p/DB51
Kansela wa Ujerumani na waziri mkuu wa LiechtensteinPicha: AP



Kashfa ya wanaokwepa kulipa kodi za mapato ,shirikisho la jamhuri ya Ujerumani yaitambua Kosovo huru na kupokonywa tawi la Ujerumani la shirika la Umoja wa mataifa linalowahudumia watoto UNICEFmhuri kuweza kukusanya misaada,ndizo mada zilizohanikiza magazetini hii leo.


Tuanze basi na kupokonywa mhuri tawi la UNICEF la Ujerumani.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linahisi taasisi kuu ya Ujerumani inayosimamia masuala ya jamii imepitisha uamuzi wa maana.Gazeti linaendelea kuandika:



"Baadhi ya wakati uamuzi mkali huhitajika hadi watu wanapotanabahi kua kweli makosa yametendeka.UNICEF ni shirika linalopendwa,linawavutia wengi wanaojitolea kulifanyia kazi na linawaleta pamoja watu kadhaa mashuhuri wanaojitolea kufanya la maana kwa kueneza ujumbe wa UNICEF.Utayarifu huo mkubwa wa kusaidia ni wa aina pekee na unawashurutisha wadhamini wasimamie misaada ya fedha inayotolewa kwa uaminifu mkubwa .Na hapo ndipo wajib wa wanaokusanya fedha ulipoingia dowa.Walifanya uzembe na ndio maana wanaadhibiwa."



Hayo ni maoni ya gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG.DIE LUÜNEBURGER LANDESZEITUNG linasema shirika hilo la misaada linakabiliwa na wakati mgumu.Gazeti linaendelea kuandika:


"Tawi la UNICEF la Ujerumani linakurubia kuangamia.Hata kama viongozi wake wote watajiuzulu-haitasaidia kitu.Kwasababu shirika hilo limejipotezea milki kubwa iliyokua nayo -uaminifu.Hata kama hadaa na udanganyifu ni kawaida kushuhudiwa katika baadhi ya mashirika,lakini UNICEF si shirika la kawaida."



Mada ya pili magazetini inahusu ziara ya waziri mkuu wa Liechtenstein,Otmar Hasler mjini Berlin.Gazeti la REINISCHEN POST la mjini Düsseldorf linasema ziara hii inagubikwa na kashfa mpya ya kodi ya mapato.Gazeti linaendelea kuandika:



"Ingawa Angela Merkel hakumuonya moja kwa moja Otmar Hasler,,hakua ta kulipiza kisasi zitachukuliwa.Lakini werevu mkubwa amekumbusha kansela Angela Merkel kwamba mpango wa Liechtenstein wa kujiunga na mkataba wa Schengen utabidi uidhinishwe bungeni.Wakati huo bila ya shaka litazuka suala vipi Liechtenstein inafikiria kushirikiana na Ujerumani katika masuala mengineyo."


Gazeti linalochapishwa ULM-SÜDWEST PRESEE linakumbusha Liechtenstein sio pepo pekee ya wanaokwepa kulipa kodi.Gazeti linaendelea kuandika:


Hasira ambazo ni za haki zitakapotulia,ndipo nao mawaziri wa fedha wa serikali kuu na majimbo watakapoweza pengine kutathmini matatizo mengine yaliyopo.Na matatizo hayo bila shaka hayahusiani pekee na Liechtenstein,bali pia Austria,Uswisi,au Monaco,yanahusiana pia na Hongkong,Singapur au visiwa vya Cayman."


Ujerumani imeitambua Kosovo,kua ni dola huru.Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:


"Si vibaya kuona kwamba Ujerumani imesubiri kidogo kabla ya kuitamabua Kosovo.Knyume kabisa. Ujerumani ilipoitambua Kroatia,miaka 16 iliyopita ilitanguliza mbele hisia "za urafiki kati ya jamii"-kabla ya kujitenganisha baadae na makosa yaliyofanywa na rafiki wepya.Safari hii ni bora zaidi.Hata mjini Belgrade viongozi watatambua kwamba dhana zao kwamba Ujerumani haiwapendi waserbia na badala yake inawapendelea waalbania hazina msingi.