1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri.

Mtullya, Abdu Said10 Aprili 2008

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wanatoa maoni yao juu ya mwenge wa olimpiki na juu ya kashfa inayohusu mafunzo yaliyotolewa kwa polisi wa Libya na maafisa wa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/DfSg
Kiongozi wa Libya M.GaddafiPicha: picture-alliance/ dpa


Wajerumani bado wanajadili mkasa unaohusu mafunzo yaliyotolewa na maafisa Ujerumani kwa  polisi wa Libya. Serikali ya Ujerumani imejitetea kwa kusema kuwa mafunzo hayo yalitolewa na  kampuni ya watu binafsi. Lakini juu ya  hayo mhariri wa gazeti la RHEIN-NECKER anauliza kwa nini hapakutolewa taarifa yoyote.? 

Masuala  mengine yanayozungumziwa na wahariri  leo ni juu ya Irak ,na wasiwasi uliopo nchini Ujerumani  juu ya kiwango cha elimu miongoni mwa baadhi ya vijana.


Na gazeti  la BERLINER ZEITUNG linazungumzia juu ya mwenge wa olimpiki.  Gazeti hilo linasema maandamano yanayofanyika kupinga mwenge wa olimpiki, hayaelekezwi tu dhidi ya  kukiukwa haki  za binadamu nchini  China. Mhariri anaeleza kuwa maandamano hayo yanaonesha taharuki iliyopo juu ya sera ya dunia utandawazi ambayo ,kwa mtazamo wa nchi za magharibi inawakilishwa kwa uthabiti na China.

Aghalabu China inaonekana kuwa  tishio na  mshindani mkali katika kuwania raslimali kama  ,vile mafuta  na  madini.

Mhariri  wa  gazeti la BERLINER ZEITUNG anaeleza katika maoni yake kuwa nchi  za magharibi  zina wasiwasi juu ya China.

Gazeti hilo linamaliza maoni yake  kwa kusema kwamba mayowe yanayopigwa juu ya kukiukwa haki  za binadamu nchini China,ni usafidi-ni kisingizio cha kusema  kuwa China imo njiani  kuzipita nchi za   magharibi katika kuidhibiti dunia mnamo  karne  hii.

Magazeti ya Ujerumani leo pia yanazungumzia juu ya Irak.

Gazeti la Swäbische Zeitung  linasema katika maoni yake, Marekani lazima ifafanue vizuri  malengo yake  nchini Irak ,la sivyo kinachotokea  sasa  kitageuka kuwa  zoezi la kudumu.

Gazeti linasema  ukweli, ni kwamba Irak haitakuwa kigezo cha  demokrasia.

Kinachotakiwa,gazeti linasema, ni kuhakikisha  kuwa nchi hiyo haigeuki kuwa tishio kwa jirani zake.

Lakini hayo yanaweza kufikiwa kwa mapatano baina ya Irak na jirani zake.

Gazeti linasema mtu yeyote  kutoka  nje, hatasaidia.

Gazeti la CELLESCHE ZEITUNG

linasisitiza  yaliyosemwa  na shirika la ushirikiano wa  kiuchumi  na  maendeleo OECD , kuwa Ujerumani  inapaswa kufanya mageuzi katika sekta ya elimu. Gazzeti  hilo linatilia maanani kwamba Ujerumani inapuuza  mustakabal  wake kutokana na sera hafifu  ya  elimu.

Gazeti linasema viwanda na  mashirika yanalalamika kuwa vijana wengi hawawezi  kusoma  na kandika vizuri.

Kutokana na  hali hiyo  gazeti  la CELLESCHE ZEITUNG linaitaka serikali   iekeze  fedha zaidi katika sekta ya elimu-

kwani huo ndiyo msingi wa maendeleo ya siku za usoni.