1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama Uingereza kusikiliza hoja kupeleka wahamiaji Rwanda

Zainab Aziz
9 Oktoba 2023

Wanasheria wa serikali leo wanatarajiwa kuiomba mahakama ya juu ya Uingereza iutengue uamuzi mahakama kuu iliyotangaza kuwa mpango wa serikali wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda ulikuwa ni kinyume cha sheria.

https://p.dw.com/p/4XHrk
Waandamanaji wakipenga uamuzi wa serikali kuwapeleka wasaka hifadhi Rwanda
Waandamanaji wakipenga uamuzi wa serikali kuwapeleka wasaka hifadhi RwandaPicha: Niklas Halle'n/AFP/ Getty Images

 Mpango huo ni miongoni mwa sera muhimu za Waziri Mkuu Rishi Sunak.

Mnamo mwezi Juni, Mahakama ya Rufaa ya mjini London iliamua kuwa mpango huo wa kuwapeleka maelfu ya wahamiaji katika taifa hilo la Afrika Mashariki haukuwa halali, ikisema Rwanda haiwezi kuchukuliwa kuwa ni nchi ya tatu salama.

Soma pia:

Mahakama hiyo ilisema kuwa wahamiaji watakaopelekwa Rwanda watakabiliwa na hatari ya kurudishwa nyumbani ambako wangeweza kukabiliwa na mateso licha ya kuwa na madai halali ya kuomba hifadhi.