1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Juu yasimamisha uchaguzi wa marudio Liberia

Isaac Gamba
7 Novemba 2017

Mahakama ya juu nchini Liberia imesimamisha duru ya pili ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika leo hadi pale tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo itakapokuwa imechungunza madai juu ya kasoro zilizojitokeza.

https://p.dw.com/p/2nA57
Liberia Präsidentin Ellen Johnson Sirleaf
Picha: dapd

Mahakama ya juu nchini Liberia imesimamisha duru ya pili ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika leo hadi pale tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo itakapokuwa imechungunza madai ya kuwepo kwa kasoro pamoja na udanganyifu katika uchaguzi wa awali. Isaac Gamba anaarifu zaidi katika taarifa ifuatayo.

Jaji Mkuu Francis Saye Korkop amesema hapo jana kuwa  tume ya taifa ya uchaguzi ilikuwa inafanya makosa    na kinyume cha sheria kusimamia uchaguzi wa marudio kati ya nyota wa zamani wa kimataifa wa kandanda George Weah  na Makamu wa wa Rais Joseph Boakai wakati kukiwa bado na malalamiko kuhusiana na uchaguzi wa awali uliofanyika mwezi Oktoba.

Wagombea hao wawili waliokuwa wakitarajiwa kuchuana kuwania nafasi itakayoachwa wazi na  rais wa kwanza mwanamke barani Afrika  hakuna hata mmoja wao aliyepata zaidi ya asilimia 50 kushinda moja kwa moja uchaguzi huo.

 Chama cha Liberty, ambacho mgombea wake Charles Brumskine alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa awali kilikata rufaa mahakamani kikitaka kusimamishwa uchaguzi wa marudio  hadi pale madai ya kuwepo kasoro katika uchaguzi huo yatakapochunguzwa.

 

Uchaguzi wa awali wadaiwa kugubikwa na kasoro

Libera, Charles Brumskine
Mgombea wa chama cha liberty nchini Liberia Charles Brumskine Picha: picture-alliance/dpa/A.Jallanzo

Brumskine pamoja na chama chake wanahoji kuwa uchaguzi wa Oktoba 10 uligubikwa  na udanganyifu na kuitaka mahakama kuiamuru tume ya uchaguzi kuchunguza malalamikoyao.

Matayarisho kwa ajili ya uchaguzi wa marudio uliokuwa umepangwa kufanyika leo Novemba 7, yaliyoyokuwa yameimamishwa  kusubiri uamuzi wa mahakama sasa yamesiamishwa moja kwa moja hadi itakapotangazwa tena.

Wakili wa tume ya uchaguzi nchini humo  Musa Dean  alilieleza shirika la habari la Associated Press kuwa  mahakama ya juu imeamua na hivyo wanapaswa kutekeleza uamuzi huo.

Jaji Mkuu Korkopr amethibitisha kuwa tarehe ya uchaguzi wa marudio haitapangwa hadi pale tume ya uchaguzi nchini humo itakapokuwa imeshuhughulikia malalamiko ya kasoro zilizowasilishwa mahakamani na chama cha Liberty.

Brumskine hapo jana amesema  chama cha Liberty hakina imani na uwezo wa tume ya uchaguzi kuchunguza malalamiko yake na kuwa hivi karibuni kitashauri  viongozi wa tume hiyo wajiuzulu.

 Tume ya uchaguzi nchini humo inakanusha kuwepo  kasoro katika uchaguzi huo na kusema uchaguzi ulifanyika katika mazingira huru na haki huku waangalizi wa kimataifa wakisema hawakuona matatizo makubwa katika uchaguzi huo.

Hata hivyo vyama kadhaa vimeonesha mashaka kuhusiana na uchaguzi  wa awali ikiwa mi pamoja na chama tawala  cha makamu wa rais Boakai ambacho wiki iliyopita kilimshutumu rais anaye ondoka madarakani Ellen Johnson Sirleaf ambaye pia ni mmoja wa wanachama wake kwa kujaribu kuwa na ushawishi katika matokeo ya uchaguzi huo madai ambayo mwanasiasa huyo ameyakanusha.

Fussball WM 2010  Qualifikationsgruppen - Auslosung Georg Weah
George Weah mgombea wa chama cha CDCPicha: picture-alliance/dpa/Pressefoto ULMER/M. Ulmer

Janga Kawo ambaye ni Katibu Mkuu wa chama cha George Weah cha CDC alitoa mwito kwa wafuasi wa chama hicho kuendelea kuwa watulivu na kuacha mahakama ifanye kazi yake huku chama cha Unity hakikuwa na kauli ya mara moja kuhusiana na uamuzi huo wa mahakama ya juu.

 Hatua ya kuchelewesha uchaguzi nchini humo imezidisha mivutano ambako wengi wanashauku yamabadiliko baada ya utawala wa miaka 12 ya Johnson Sirleaf.

Mwandishi: Isaac Gamba/rtre/ape

Mhariri: Josephat Charo