1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mahakama ya rufaa: Trump hana kinga ya kutoshtakiwa

7 Februari 2024

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, hana kinga ya kutoshtakiwa na anaweza kuhukumiwa kwa tuhuma za kula njama ya kujaribu kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.

https://p.dw.com/p/4c7Gf
New York | Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akielekea katika Mahakama ya mjini New York kusikiliza kesi dhidi yake: 26.01.2024Picha: Charly Triballeau/AFP/Getty Images

Uamuzi huo wa kihistoria umetolewa mjini Washington na Majaji watatu wa Mahakama ya rufaa ya shirikisho.

Majaji hao wamesema hoja ya Trump ya kwamba anayo kinga ya kutoshtakiwa kwa hatua zote alizozichukua akiwa kama rais, haina mashiko na kwamba inakinzana na historia, misingi ya katiba ya Marekani na kwamba hatua kama hiyo ingedhoofisha mfumo wa mihimili mitatu ya uongozi.

Muda mfupi baada ya uamuzi huo, msemaji wa timu ya  kampeni ya Trump , Steven Cheung amesema rais huyo wa zamani "hakubaliani kabisa na uamuzi huo na kwamba atakata rufaa katika Mahakama ya Juu ya Marekani.