1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya The Hague ,yaisafisha Serbia

Charles Mwebeya26 Februari 2007

Mahakama ya kimataifa ya The Hague nchini Uholanzi ,imesema Serikali ya Serbia haikuhusika moja kwa moja na mauaji ya halaiki ya mwaka 1995 katika vita dhidi ya Bosnia.

https://p.dw.com/p/CHJK
Baadhi ya mawakili wa Bosnia wakiwa mahakamani katika kesi yake dhidi ya Serbia huko , The Hague .
Baadhi ya mawakili wa Bosnia wakiwa mahakamani katika kesi yake dhidi ya Serbia huko , The Hague .Picha: AP

Mahakama hiyo imetoa uamuzi huo katika kesi ya kwanza ya mauaji ya mwaka 1995.

Endapo Bosnia ingeshinda kesi hiyo dhidi ya Serbia , Serbia ingelazimika kuilipa Bosnia mabilioni ya Dolla kama fidia.

Jaji Rosalyn Higgins amesema mahakama imebaini kuwa mauaji ya mwaka 1995 huko Sebrenica yalikuwa mauaji ya halaiki na Serbia ilishindwa kuchukua hatua dhidi yake ,lakini hayaihusishi serikali ya Serbia moja kwa moja.

Karibu watu laki moja wanasadikiwa kupoteza nmaisha katika vita ya mwaka 1992-1995 wakati waumini wa dini ya kiislamu wa Bosnia na Croatia walipotaka kujitenga na Yugoslavia hatua iliyopingwa vikali na Waserbia wa Bosnia.

Miili ya watu zaidi ya 80 ilipatikana ikiwa imefukiwa katika makaburi ya pamoja huku wengi wao wakiwa ni waumini wa kiislam kutoka Bosnia.

Serbia kwa upande wake imesema uamuzi huo utathibitisha dhana iliyopo , ambayo ilisababisha mtawala wake Slobodan Milosevic kuondolewa madarakani mwaka 2000.

Bosnia ambayo kwa sasa imegawanyika pande mbili kati ya shirikisho la kiislam la Crooatia na Jamhuri ya Serbia, hisia imejengeka hususani kwa waumini wa dini ya kiislam ambao wanatazamia mahakama ya kimataifa kuimbua Serbia.

Kabla mahakama haijatoa uamuzi wa kesi hiyo, takribani watu 50 walikuwa wakifanya maandamano nje ya jengo la mahakama hiyo.

Hedija Kerzich mwanamke aliyempoteza mume wake katika mauaji hayo alisema uamuzi wa kuitia hatiani Sebia ungekuwa na umuhimu mkubwa kwake.

Ni takribani miaka 14 imepita toka Bosnia ilipoushtaki utawala wa iliyokuwa Yugoslavia, baada ya kujitenga mnamo mwaka 1992.

Mahakama ya Kimataifa ya The Hague imesema imepata ushahidi unaowaweka hatiani baadhi ya viongozi wa zamani wa Serbia na siyo serikali kwa ujumla .

Mmoja wa viongozi wa serikali ya zamani ya Kosovo Ramush Haradinaj ameondoka Pristina hii leo kuelekea Uholanzi ambako atasomewa mashtaka dhidi ya mauaji hayo , March 05 mwaka huu.

Haradinaj anakabiliwa na tuhuma za kuhusika katika kupanga mauaji, ubakaji na mateso katika vita hiyo .

Rais wa zamani wa iliyokuwa Yugoslavia Slobodan Milosevich alifariki dunia mwaka jana kabla ya kutolewa hukumu yake , akikabiliwa na mashtaka 66 ya mauaji pamoja na makosa ya kivita katika kesi hiyo.

Kuibuka kwa mgawanyiko kati ya waislam wa Bosnia na Croatia kulifuatia Slovenia na Croatia kujitoa katika muungano na Yugoslavia mwezi April mwaka 1992, dhidi ya matakwa ya Waserbia wenye asili ya Bosnia na kupelekea vita na mauaji makubwa yaliyosababisha watu laki moja kupoteza maisha.

.