1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Mahakama ya Uchaguzi Pakistan yaamuru kuharakishwa matokeo

Lilian Mtono
9 Februari 2024

Uhesabuji kura nchini Pakistan umekumbwa na ucheleweshwaji usio wa kawaida, hali iliyosababisha Mahakama ya Uchaguzi kuwataka maafisa wa tume ya uchaguzi kuwasilisha matokeo mara moja.

https://p.dw.com/p/4cD6L
Maafisa uchaguzi wakimimina kura kwa ajili ya kuzihesabu nchini Pakistan.
Maafisa uchaguzi wakimimina kura kwa ajili ya kuzihesabu nchini Pakistan.Picha: NAVESH CHITRAKAR/REUTERS

Onyo hilo lilitolewa masaa 10 baada ya kufungwa kwa vituo vya uchaguzi.

Mmoja ya maafisa maalumu kwenye Tume ya Uchaguzi ya Pakistan (ECP), Zafar Iqbal, amesema baada ya kutangaza matokeo ya kwanza ya majimbo masaa 10 baada ya uchaguzi, changamoto ya mtandao ndio imesababisha kuchelewa huko.

Soma zaidi: Pakistan yaanza kuhesabu kura baada ya uchaguzi kukamilika

Ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya wagombea wanaoungwa mkono na waziri mkuu wa zamani aliyeko gerezani, Imran Khan, na chama cha Pakistan Muslim League ambacho pia ni cha waziri mkuu wa zamani, Nawaz Sharif.

Picha halisi ya matokeo inatarajiwa kuanza kujitokeza leo Ijumaa (Februari 9) baada ya zoezi la kuhesabu kuendelea usiku kucha.